Nenda kwa yaliyomo

Humphrey Polepole

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Humphrey Herson Polepole
Muda wa Utawala
2022  13 Julai 2025

tarehe ya kuzaliwa 1980
Tanzania
utaifa Mtanzania
chama Chama Cha Mapinduzi
dini Mkristo

Humphrey Herson Polepole (alizaliwa 1980) ni mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Tanzania ambaye alihudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Malawi, halafu nchini Kuba kuanzia 2023 hadi alipojiuzulu tarehe 13 Julai 2025.[1] Hapo awali alihudumu kama Kamishna Mkuu wa Tanzania nchini Malawi kuanzia 2022 hadi 2023.[2]

Alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi na Mbunge wa kuteuliwa na Rais John Magufuli.[3]Kabla ya kuteuliwa Humphrey Polepole alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa muda wa miezi mitano, pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma kwa miezi miwili.

Tarehe 5 Agosti 2025 serikali ilitoa barua ya kumvua Polepole hadhi ya balozi. Barua ambayo ilitolewa na serikali ilidai kumvua cheo hicho tangu Julai 16 2025.[4]

  1. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/national/polepole-resigns-from-diplomatic-role-cites-leadership-concerns-as-ccm-responds-5116550
  2. https://www.tzembassy.go.tz/ambassadors/view/humphrey-polepole
  3. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/national/polepole-resigns-from-diplomatic-role-cites-leadership-concerns-as-ccm-responds-5116550
  4. "Rais Samia atengua uteuzi wa Polepole, amuondolea hadhi ya ubalozi". BBC News Swahili. 2025-08-05. Iliwekwa mnamo 2025-08-23.
Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Humphrey Polepole kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.