Hugolino wa Montegiorgio

Hugolino wa Montegiorgio (1255/1260 - 1344/1348) alikuwa mtawa na mwandishi wa shirika la Ndugu Wadogo maarufu kwa kutunga (1328 hivi[1]) kitabu “Actus” (= “Matendo” ya Fransisko na wenzake) ambacho kikatafsiriwa kwa Kiitalia mwishoni mwa karne ya 14[2].
Tafsiri hiyo, yenye jina la “Fioretti” (= “Maua Madogo”, yaani “Visimulizi Bora”), ikasifiwa sana kwa uzuri wake, ingawa visimulizi vyake si vyote vya kihistoria. Ni kama manukato yanayovutia kwenye roho na utakatifu wa Fransisko wa Asizi, aliyekwishafariki dunia toka siku nyingi, hivi kwamba anakumbukwa kwa mbali lakini kwa namna ya kupendeza zaidi. Miaka iliyopita imechuja ujumbe wake, ambao hivyo unang’aa kwa namna ya pekee katika kitabu hicho kilichosisitiza jinsi Fransisko alivyofanana na Yesu, wazo lililokazwa na Wafransisko wote wa karne hiyo, hasa na Bartolomayo wa Pisa, mwandishi wa “Conformitates” (= “Uwiano Mwingi”)[3].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ (Kiingereza)Life of St. Francis of Assisi.
- ↑ (Kiingereza)Ugolino Brunforte.
- ↑ (Kiingereza)Fioretti di San Francesco.
Sehemu kubwa ya Fioretti kwa Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Fioretti – Visimulizi Kuhusu Mtakatifu Fransisko wa Asizi – tafsiri ya Rikardo Maria, U.N.W.A. n.k. – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1996 – ISBN 9976-63-468-4
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Luca Wadding, Scriptores Ordinis Minorum (1650), 179
- Giovanni Giacinto Sbaraglia, Supplementum et castigatio ad scriptores trium ordinum S. Francisi (8106), addenda 727
- Luigi da Fabriano, Disquisizione istorica intorno all' autore dei Fioretti (Fabriano, 1883)
- Cenni cronologico-biografici dell'osservante Provincia Picena (Quaracchi, 1886), 232 sqq.
- Alessandro Manzoni, Fioretti (2nd ed., Rome, 1902), prefazione
- Candido Mariotti, I Primordi Gloriosi dell'ordine Minoritico nelle Marche (Castelplanio, 1903), VI
- (Kiingereza) Arnold, The Authorship of the Fioretti (London, 1904)
- Camillo Pace, "L'autore del Floretum in Rivista Abruzzese", ann. XIX, fasc. II
- François Van Ortroy, in Analecta Bollandiana, XXI, 443 sqq.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza)The Little Flowers of Saint Francis.