Hospitali ya Machame

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mnamo octoba 1893 mtemi Shangali wa kabila la wachaga pamoja na watu wa kabila lake walikaa chini ya mti katika mlima Kilimanjaro katika eneo la Nkwarungo pamoja na wamisionari wa ujerumani kutoka Leipzig. Wamisionari waliwatibu vidonda vya tumbo na vidonda vya ngozi. Mpaka hii leo huduma hii inaendelea.

Mnamo mwaka 1906 dokta Herman Ploetze alifika Machame kama daktari wa kimisionari na kupanga ujenzi wa mwanzo wa hospitali ya kilutheri ya Machame. Hospital ilibadilika na kukua ndani ya miaka 100. Kwa miaka mingi hospitali iliongozwa na huduma nyingi kutolewa na madaktari wa kijerumani. Watanzania pamoja na watu wan chi zingine waliweza kutoa huduma vilevile. Mtanzania wa kwanza kutoa huduma alikuwa ni dokta Iraeli S.Moshi mwaka 1976.

Hospitali hii ilihudumu kama hospitali ya mwanzo ya rufaa na utabibu kaskazini mwa Tanzania na maeneo ya karibu ikiwa na zaidi ya vitanda 200. Hospitali zingne zilijengwa vilevile na Machame imekuwa na kufikia jumla ya vitanda 130 vya upasuaji na kuhudumia jamii ya Kilimanjaro.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-12. Iliwekwa mnamo 2020-03-07. 
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hospitali ya Machame kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.