Hospitali ya Taifa ya Kenyatta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hospitali ya Kenyatta

Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta iliyoko jijini Nairobi, ni Hospitali kongwe zaidi nchini Kenya. Ilianzishwa mwaka wa 1901 na uwezo wa vitanda takribani 40 kama Native Civil Hospital, ilibadilishwa jina na kuitwa King George VI mwaka 1952. Wakati huo,masetla walikuwa wakihudumiwa na hospitali ya jamii iliyoko karibu, European Hospital (sasa inaitwa Nairobi Hospital). Ilibadilishwa jina hadi Kenyatta National Hospital - baada ya Jomo Kenyatta - kufuatia uhuru kutoka Uingereza. Kwa sasa ndiyo hospitali kubwa ya rufaa na mafundisho nchini.

Kenyatta National Hospital ina uwezo wa vitanda 1800 na ina wafanyakazi zaidi ya 6000. Ipo kwenye eneo la hekta 45.7. Shule ya Udakitari ya Chuo Kikuu cha Nairobi, na mashirika kadhaa ya serikali yako hapa.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hospitali ya Taifa ya Kenyatta kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.