Hospitali ya Butabika
Hospitali ya Butabika (Butabika Hospital) ni hospitali ya afya ya akili iliyoko Kampala, Uganda. Ni mojawapo ya hospitali chache katika Afrika Mashariki zinazotoa buprenofini. Buprenofini ni dawa yenye ufanisi mkubwa katika matibabu ya uraibu wa opiati. Hospitali hii pia ni hospitali ya mafunzo ya magonjwa ya akili kwa Chuo cha Sayansi za Afya cha Chuo Kikuu cha Makerere.
Matibabu ya Uraibu
[hariri | hariri chanzo]Butabika ilikuwa ikitoa methadoni na ushauri tu kwa matibabu ya uraibu wa opiati. Mnamo mwaka wa 2020, Butabika ilianzisha programu yake ya kwanza ya buprenofini. Polepole, wagonjwa watatu tu walikamilisha programu hiyo. Kwa sababu Butabika iliwahitaji wagonjwa kutembelea kliniki ya buprenofini kila siku kuchukua dawa zao, wagonjwa walikumbana na changamoto za kufika kwa miadi yao. Kwa sababu ya changamoto hii, Butabika iliruhusu baadhi ya wagonjwa kuchukua dawa zao nyumbani. Kwa kuwa buprenofini ni dawa yenye ufanisi mkubwa, ni muhimu kwamba wagonjwa wasikabiliane na changamoto za kupata dawa hii.
Shule ya Maafisa wa Kliniki ya Magonjwa ya Akili
[hariri | hariri chanzo]Hospitali ya Butabika pia ni makao ya Shule ya Maafisa wa Kliniki ya Magonjwa ya Akili. Hii ni shule inayoendeshwa na Wizara ya Afya ya Uganda, ambayo huwafundisha wahitimu wa shule za sekondari kuwa Maafisa wa Kliniki wa Magonjwa ya Akili. Ni shule ya pekee ya aina yake katika Afrika Mashariki.
Changamoto za Butabika
[hariri | hariri chanzo]Butabika ni hospitali ya pili kwa ukubwa nchini Uganda, ikiwa na uwezo wa vitanda mia tano na hamsini, ingawa idadi ya wagonjwa mara nyingi hutofautiana kati ya mia nane na hamsini hadi elfu moja. Hospitali pia inashughulikia idara ya wagonjwa wa nje yenye shughuli nyingi, na hupokea takriban wateja mia tatu na hamsini kwa siku katika maeneo ya huduma za afya ya jumla na afya ya akili.
Kwa sababu kuna wagonjwa wengi kuliko vitanda hospitalini, kuna matatizo ya msongamano.
Kulikuwa na ripoti kuhusu msongamano huo mwaka 2024. Kulingana na ripoti hiyo, wodi za hospitali zilipatikana kuwa chafu, zimejaa watu kupita kiasi, na hazikuwa na ulinzi wa kimsingi wa hadhi ya binadamu. Katika wodi kadhaa, kulikuwepo na ushahidi wa utapiamlo, na wagonjwa wengi walikuwa na matatizo ya ngozi, vidonda, na usafi duni kwa jumla. Watoto walipatikana wakilazwa pamoja na watu wazima, na wagonjwa wenye hali mbaya za afya waliachwa bila matibabu. Kwa bahati nzuri, ripoti hii ilihusu tu hali ya matibabu ya wagonjwa wa kulazwa. Wagonjwa wa nje hawatendewi vibaya kiasi hicho.
Butabika inahitaji kupanua miundombinu yake, kutoa vitanda zaidi, na kuboresha matibabu kwa wagonjwa wanaoishi hospitalini.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- https://hri.global/wp-content/uploads/2022/11/GSHR-2022_Eastern-and-Southern-Africa.pdf
- https://www.butabikahospital.go.ug/news-old/14-report-questions-handling-of-patients-in-butabika Ilihifadhiwa 29 Aprili 2025 kwenye Wayback Machine.
- https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC9407835/
- https://observer.ug/news/withdrawal-of-pepfar-leaves-drug-use-intervention-effort-in-deep-crisis/