Nenda kwa yaliyomo

Homo longi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fuvu la kichwa la Harbin, kielelezo cha Homo longi.
Uenezi wa jenasi Homo kwa wakati na mahali kuanzia miaka 2,000,000 iliyopita.
Uenezi na mageuko ya Wadenisova.

Homo longi (pia: Wadenisova) katika uainishaji wa kisayansi ni jina mojawapo lililopendekezwa kwa spishi au nususpishi iliyokoma ya zamadamu[1][2][3] ambayo imekadiriwa kuanza kuwepo miaka laki 4 hivi iliyopita huko Eurasia kutokana na Homo heidelbergensis na kisha kutofautiana na jamaa zao wa jirani, Homo neanderthalensis[4]. Ingawa Homo longi alielekea mashariki na Homo neanderthalensis magharibi, wataalamu wanazidi kuthibitisha kwamba hao walizaliana kati yao (kwa mfano katika pango la Denisova)[5], halafu na Homo sapiens aliyetoka nje ya Afrika miaka 50,000 hivi iliyopita, wakirithisha baadhi ya jeni zao kwa watu wa leo, hasa wasio wa Kusini kwa Sahara.

Kwa namna ya pekee jeni za Homo longi zinapatikana katika wakazi asili wa Ufilipino, Guinea Mpya na Australia[6], lakini pia wa Asia mashariki na Amerika[7] .

  1. Fu, Q.; Bai, F.; Rao, H.; Chen, S.; Ji, Y.; Liu, A.; Bennett, E. A.; Liu, F.; Ji, Q. (2025). "The proteome of the late Middle Pleistocene Harbin individual". Science. 389 (6761) eadu9677. Bibcode:2025Sci...389..704F. doi:10.1126/science.adu9677. PMID 40531192.
  2. Fu, Q.; Cao, P.; Dai, Q.; Bennett, E. A.; Feng, X.; Yang, M. A.; Ping, W.; Pääbo, S.; Ji, Q. (2025). "Denisovan mitochondrial DNA from dental calculus of the >146,000-year-old Harbin cranium". Cell. 188 (15): 3919–3926.e9. doi:10.1016/j.cell.2025.05.040. PMID 40920634.
  3. Curry, Andrew (18 Juni 2025). "'Dragon Man' skull belongs to mysterious human relative". Science. American Association for the Advancement of Science (AAAS). doi:10.1126/science.z8sb68w.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Gokhman, David; Mishol, Nadav; de Manuel, Marc; de Juan, David; Shuqrun, Jonathan; Meshorer, Eran; Marques-Bonet, Tomas; Rak, Yoel; Carmel, Liran (2019-09-19). "Reconstructing Denisovan Anatomy Using DNA Methylation Maps". Cell. 179 (1): 180–192. doi:10.1016/j.cell.2019.08.035. PMID 31539495.
  5. Warren, M. (2018). "Mum's a Neanderthal, Dad's a Denisovan: First discovery of an ancient-human hybrid – Genetic analysis uncovers a direct descendant of two different groups of early humans". Nature. 560 (7719): 417–418. Bibcode:2018Natur.560..417W. doi:10.1038/d41586-018-06004-0. PMID 30135540.
  6. Larena, M.; McKenna, J.; Sanchez-Quinto, F.; Bernhardsson, C.; Ebeo, C.; Reyes, R.; Casel, O.; Huang, J.-Y.; Hagada, K. P.; Guilay, D.; Reyes, J.; Allian, F. P.; Mori, V.; Azarcon, L. S.; Manera, A.; Terando, C.; Jamero Jr., L.; Sireg, G.; Manginsay-Tremedal, R.; Labos, M. S.; Vilar, R. D.; Latiph, A.; Saway, R. L.; Marte, E.; Magbanua, P.; Morales, A.; Java, I.; Reveche, R.; Barrios, B.; Burton, E.; Salon, J. C.; Kels, Ma. J. T.; Albano, A.; Cruz-Angeles, R. B.; Molanida, E.; Granehäll, L.; Vicente, M.; Edlund, H.; Loo, J.-H.; Trejaut, J.; Ho, S. Y. W.; Reid, L.; Lambeck, K.; Malmström, H.; Schlebusch, C.; Endicott, P.; Jakobsson, M. (11 Oktoba 2021). "Philippine Ayta possess the highest level of Denisovan ancestry in the world". Current Biology. 31 (19): 4219–4230.e10. Bibcode:2021CBio...31E4219L. doi:10.1016/j.cub.2021.07.022. PMC 8596304. PMID 34388371.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Prüfer, K.; Racimo, F.; Patterson, N.; Jay, F.; na wenz. (2013). "The complete genome sequence of a Neanderthal from the Altai Mountains". Nature. 505 (7481): 43–49. Bibcode:2014Natur.505...43P. doi:10.1038/nature12886. PMC 4031459. PMID 24352235.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homo longi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.