Homo habilis
Homo habilis (maana ya Kilatini ni "mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vifaa") katika uainishaji wa kisayansi ni spishi iliyokoma ya zamadamu wa kwanzakwanza[1][2]. Mabaki yake yalipatikana huko Oltupai (Tanzania). Huyo anafikiriwa kutokana na Australopithecus garhi ambaye kabla yake alikuwa ameanza kutengeneza vifaa kwa mawe. Pia kwa sababu hiyo, kwamba hakuwa kiumbehai wa kwanza kutengeneza vifaa, baadhi ya wanasayansi wamependekeza jina lake liwe "Australopithecus habilis"[3][4][5][6].
Tena mnamo Mei 2010 huko Afrika Kusini yalipatikana mabaki ya Homo gautengensis, spishi inayofikiriwa na wengine kuwa ya kale kuliko Homo habilis[7], lakini wengine wanaijumlisha katika jina Homo habilis. Kumbe wataalamu wengine wanaona spishi hizo mbili hazistahili kuitwa Homo, ila Australopithecus.
Historia ya awali
[hariri | hariri chanzo]
Spishi hiyo [8] imekadiriwa kuanza kuwepo miaka milioni 2.4 iliyopita[9][10] kutokana na spishi mojawapo ya nusukabila Australopithecina (siku hizi linatumika pia jina Hominina) iliyokuwepo kuanzia miaka milioni 5.6 hadi 1.2 iliyopita. Homo habilis alikoma miaka milioni 1.65 iliyopita.
Kutokana naye alipatikana miaka milioni 2 iliyopita Homo erectus aliyekuwa wa kwanza kusimama daima juu ya miguu yake miwili, kuwinda na kumudu moto, na ambaye alienea kote Asia na Ulaya (aliyebaki Afrika anaitwa pia Homo ergaster) kabla ya kugawanyika katika nususpishi au spishi mpya mbalimbali kama Homo georgicus, Homo antecessor, Homo heidelbergensis, wa kwanza kujenga makazi ya kudumu na kuzika wafu, n.k. Kwa jumla Homo erectus alidumu zaidi ya miaka milioni moja. Wengi wanaona spishi nyingi zilizopendekezwa awali kuwa nususpishi tu za Homo erectus.
Miaka 800,000–200,000 iliyopita, wakati wa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, ubongo wa jenasi hiyo ulikua sana na kupata uwezo wa kufanya mambo mengi mapya katika mahusiano na katika kukabili mazingira ambayo yalizidi kubadilika na kudai maitikio tofauti ili kudumisha uhai wa jenasi yenyewe. Kwamba homo sapiens ametokana na Homo erectus moja kwa moja ni dhana inayozidi kupingwa.
Picha
[hariri | hariri chanzo]- Homo habilis mwanamume
- Homo naledi mwanamume
- Homo rudolfensis mwanamume
- Homo erectus mwanamke
- Homo floresiensis mwanamke
- Homo heidelbergensis mwanamume
- Homo longi mwanamume
- Homo luzonensis mwanamume
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Stringer, C.B. (1994). "Evolution of early humans". Katika Jones, S.; Martin, R.; Pilbeam, D. (whr.). The Cambridge Encyclopedia of Human Evolution. Cambridge: Cambridge University Press. uk. 242.
- ↑ Schrenk, F.; Kullmer, O.; Bromage, T. (2007). "Chapter 9: The Earliest Putative Homo Fossils". Katika Henke, W.; Tattersall, I. (whr.). Handbook of Paleoanthropology. ku. 1611–1631. doi:10.1007/978-3-540-33761-4_52.
- ↑ Wood, B.; Collard, M. (1999). "The Human Genus" (PDF). Science. 284 (5411): 65–71. Bibcode:1999Sci...284...65.. doi:10.1126/science.284.5411.65. PMID 10102822. S2CID 7018418. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-11-23.
- ↑ Miller J. M. A. (2000). "Craniofacial variation in Homo habilis: an analysis of the evidence for multiple species". American Journal of Physical Anthropology. 112 (1): 103–128. doi:10.1002/(SICI)1096-8644(200005)112:1<103::AID-AJPA10>3.0.CO;2-6. PMID 10766947.
- ↑ Tobias, P. V. (1991). "The species Homo habilis: example of a premature discovery". Annales Zoologici Fennici. 28 (3–4): 371–380. JSTOR 23735461.
- ↑ Collard, Mark; Wood, Bernard (2015). "Defining the Genus Homo". Handbook of Paleoanthropology. ku. 2107–2144. doi:10.1007/978-3-642-39979-4_51. ISBN 978-3-642-39978-7.
- ↑ ""Toothy Tree-Swinger May Be Earliest Human"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-02. Iliwekwa mnamo 2012-04-28.
- ↑ Johanson, D. C.; Masao, F.; Eck, G. G.; White, T. D.; na wenz. (1987). "New partial skeleton of Homo habilis from Olduvai Gorge, Tanzania". Nature. 327 (6119): 205–209. Bibcode:1987Natur.327..205J. doi:10.1038/327205a0. PMID 3106831. S2CID 4321698.
- ↑ Stringer, C.B. (1994). "Evolution of early humans". The Cambridge Encyclopedia of Human Evolution. Cambridge: Cambridge University Press. uk. 242. ISBN 0-521-32370-3.
{{cite book}}: Unknown parameter|editors=ignored (|editor=suggested) (help) Also ISBN 0-521-46786-1 (paperback) - ↑ McHenry, H.M (2009). "Human Evolution". Evolution: The First Four Billion Years. Cambridge, Massachusetts: The Belknap Press of Harvard University Press. uk. 265. ISBN 978-0-674-03175-3.
{{cite book}}: Unknown parameter|editors=ignored (|editor=suggested) (help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Wikispecies has information related to: Homo habilis |
- Reconstructions of H. habilis by John Gurche
- Archaeology Info Archived 2011-05-26 at the Wayback Machine
- Homo habilis – The Smithsonian Institution's Human Origins Program
- Human Timeline (Interactive) – Smithsonian, National Museum of Natural History (August 2016).
| Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Homo habilis kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
