Nenda kwa yaliyomo

Homo ergaster

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Homo ergaster.
Uenezi wa jenasi Homo kwa wakati na mahali kuanzia miaka 2,000,000 iliyopita.

Homo ergaster (maana ya Kilatini ni "mtu anayefanya kazi"; anaitwa pia: Telanthropus capensis, Homo erectus ergaster, Homo louisleakeyi, Homo kenyaensis na Homo okotensis) katika uainishaji wa kisayansi ni spishi au nususpishi iliyokoma ya zamadamu ambayo imekadiriwa kuwepo miaka milioni 1.9 hivi hadi milioni 1.4 au 1.2 iliyopita[1] huko Afrika kutokana na Homo habilis (anayeitwa pia Australopithecus habilis). Mageuko yaliyotokea kati ya spishi hizo mbili ni hatua muhimu kuelekea Homo sapiens, kwa sababu ubongo ukawa mkubwa zaidi kidogo (hadi sentimeta za ujazo 910), na kumwezesha kutengeneza vifaa vinavyoonyesha teknolojia ya juu zaidi. Pengine anajumlishwa na mzao wake aliyetoka bara la Afrika anayeitwa Homo erectus kwa sababu alikuwa wa kwanza kusimama daima juu ya miguu yake miwili, kuwinda[2] na labda kumudu moto, kabla ya kugawanyika katika nususpishi au spishi mpya mbalimbali, hasa Homo heidelbergensis, wa kwanza kujenga makazi ya kudumu na kuzika wafu, n.k.

Wengi wanakubali Homo sapiens alitokana na Homo ergaster kupitia Homo heidelbergensis, kama ilivyotokea kwa Homo neanderthalensis na Homo longi. Ni kwamba miaka 800,000–200,000 iliyopita, wakati wa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, ubongo wa jenasi Homo ulikua sana na kupata uwezo wa kufanya mambo mengi mapya katika mahusiano na katika kukabili mazingira ambayo yalizidi kubadilika na kudai maitikio tofauti ili kudumisha uhai wa jenasi yenyewe.

  1. Wood, Bernard; Doherty, Dandy; Boyle, Eve (29 Mei 2020). "Hominin Taxic Diversity". Oxford Research Encyclopedia of Anthropology (kwa Kiingereza). doi:10.1093/acrefore/9780190854584.013.194. ISBN 978-0-19-085458-4. Iliwekwa mnamo 19 Aprili 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Ben-Dor, Miki; Sirtoli, Raphael; Barkai, Ran (2021). "The evolution of the human trophic level during the Pleistocene". American Journal of Physical Anthropology. 175 (S72): 27–56. Bibcode:2021AJPA..175S..27B. doi:10.1002/ajpa.24247. PMID 33675083.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homo ergaster kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.