Homa ya kuvuja damu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Virusi vya Marburg vinavyosababisha homa ya kuvuja damu.

Homa ya kuvuja damu (kwa Kiingereza: Marburg hemorrhagic fever au Marbur virus disease) ni ugonjwa mkali wa wanadamu na wanyama kama vile tumbili, nyani, sokwe, ambao husababishwa na virusi vya Marburg vya aina mbili.

Ugonjwa huo husababishwa na virusi vinavyohusianishwa na Ebola na hata dalili zake hazina tofauti kubwa na ugonjwa wa Ebola. Virusi hivyo vilitambuliwa mara ya kwanza katika mji wa Marburg, Ujerumani mnamo mwaka 1967, wakati wafanyakazi wa maabara waliambukizwa walipochungulia nyani kutoka Afrika ya Kati. Baadaye virusi hivihivi vilitambuliwa wakati wa mlipuko wa ugonjwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo 1998 - 2000.

Dalili[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa huo huanza kwa ghafla, na homa kubwa, maumivu ya kichwa, uchovu au kuhisi vibaya mwili mzima, maumivu ya misuli ni kipengele cha kawaida. Kuharisha kwa maji mengi, maumivu ya tumbo na kichomi, kichefuchefu na kutapika kunaweza kuanza siku ya tatu. Kuhara huweza kuendelea kwa wiki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homa ya kuvuja damu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.