Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Visiwa vya Kanari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Visiwa vya Kanari na Hispania
Ramani ya Visiwa vya Kanari

Historia ya Visiwa vya Kanari inahusu funguvisiwa la Afrika ya Kaskazini katika bahari ya Atlantiki. Viko baharini km 150 magharibi kwa Moroko. Umbali na Hispania ni saa mbili kwa ndege. Kisiasa visiwa hivyo ni kati ya maeneo ya kujitawala ndani ya ufalme wa Hispania.

Visiwa vya Kanari vilitembelewa zamani na wasafiri Wafinisia, Wagiriki na Waroma, baadaye na Waarabu. Katika Ulaya visiwa vilisahauliwa hadi mwaka 1400 hivi.

Visiwa vilikaliwa na wazawa walioitwa Guancha na Wahispania walipofika Kanari. Hakuna uhakika kuhusu asili yao. Wataalamu wengi hufikiri walikuwa Waberber. Wengine husema walikuwa wafungwa walioachiwa huru visiwani wakati wa Dola la Roma.

Wakati wa kufika kwa Wahispania kuanzia mwaka 1400 walikuwa na utamaduni bila chuma; wanasemekana hawakujua usafiri wa bahari.

Katika muda wa karne moja Wahispania walivamia visiwa na kukandamiza utamaduni wa wenyeji. Lugha yao imekwisha kabisa ingawa kuna bado majina ya mahali visiwani kutokana na lugha ya Kiguancha.

Baada ya Wahispania kufika Amerika, Las Palmas ilikuwa bandari muhimu ya safari za Atlantiki.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Visiwa vya Kanari kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.