Historia ya Melilla

Historia ya Melilla (tamka: me-li-ya; kwa Kiarabu: مليلية, Meliliya; jina rasmi: Ciudad Autónoma de Melilla = Mji wa kujitawala wa Melilla) inahusu mji huo wa Afrika kwenye pwani ya Mediteranea unaozungukwa na eneo la Moroko upande wa bara. Umbali na Hispania bara ni takriban km 170 kuvuka bahari. Mji ulio karibu upande wa Moroko ni Nador kwenye umbali wa km 15. Pamoja na mji wa Ceuta kisiasa ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya, ila Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.
Historia yake ilianza zaidi ya miaka 2000 iliyopita ulipoundwa kwa jina la Rusadir. Ukawa sehemu ya Dola la Roma katika jimbo la Mauretania Tingitana. Eneo lake lilipiganiwa kuanzia mwaka 429 BK kati ya wavamizi Wavandali na Bizanti.
Kabla ya mwaka 700 Waarabu Waislamu walivamia eneo la pwani ya Moroko wakielekea Hispania. Mji ulipata jina la Meliliya ukabaki chini ya utawala wa Kiislamu hadi mwaka 1497 ulipotekwa na Wahispania.
Wahispania walifaulu kubaki na mji katika vita mbalimbali vya karne zilizofuata. Mwaka 1936 vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania vilianza Melilla kwa uasi wa wanajeshi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Hispania.
| Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Melilla kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |