Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Ceuta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ceuta na rasi yake.
Ceuta (Hispania)

Historia ya Ceuta (tamka: the-uta; kwa Kiarabu: سبتة sabta) inahusu mji huo wa Afrika kwenye pwani ya Mediteranea ambao upande wa bara unazungukwa na eneo la Moroko. Ceuta iko karibu na mji wa Tetouan upande wa Moroko. Umbali na Hispania ni km 21 kuvuka mlango wa bahari wa Gibraltar. Pamoja na mji wa Melilla ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya kisiasa, lakini Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.

Ceuta inaaminika iliundwa na Karthago katika karne ya 5 KK.

Jina la Kigiriki la mji imekuwa "Επτά Αδελφοί" (hepta adelphoí - ndugu saba). Tangu Waroma walipochukua utawala wa Afrika ya Kaskazini mji ulijulikana kwa jina la "Septem Fratres" (ndugu saba). Jina hilo limeendelea hadi leo, mji ukiitwa "sabta" kwa Kiarabu au kwa matamshi ya Kihispania "Ceuta".

Kuanzia karne ya 5 BK mji ulitawaliwa na Wavandali.

Mwaka 710 Waarabu Waislamu walifika wakipita Ceuta kuvamia Hispania.

Hadi karne ya 14 mji ulikuwa chini ya watawala Waislamu ama Waarabu au Waberberi. Kati ya Wakristo waliofia dini yao huko wanakumbukwa watakatifu Danieli mfiadini na wenzake (1226).

Mwaka 1415 Wareno waliteka Ceuta wakaitawala hadi mwaka 1668. Baada ya vita kati ya Ureno na Hispania mji ulikabidhiwa kwa mfalme wa Hispania. Hivyo tangu mwaka 1668 Ceuta imekuwa sehemu ya Hispania. Ndani ya Hispania imekuwa Mji wa kujitawala (kwa Kihispania: ciudad autónoma) tangu mwaka 1995.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Ceuta kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.