Nenda kwa yaliyomo

Hisili Music

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hisili Music ni bendi ya muziki wa asili kutoka Tanzania inayojulikana kwa kuchanganya miondoko ya hip hop na muziki wa asili. Bendi hii ilianzishwa mwaka 2023 mkoani Mbeya, katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Asili ya jina

[hariri | hariri chanzo]

Jina Hisili linatokana na muunganiko wa maneno mawili: Hip Hop na Asili, yakimaanisha mtindo wa muziki unaochanganya midundo ya kisasa na ala za kitamaduni za Kiafrika.

Mtindo wa Muziki na Ala

[hariri | hariri chanzo]

Bendi hiyo inatumia ala za muziki za asili ambazo hutengenezwa kienyeji, zikiwemo:

  • Gitaa la nyuzi tatu
  • Ngoma za jadi
  • Babatoni (aina ya besi ya kitamaduni)
  • Midundo ya banjo

Wasanii wa bendi ya Hisili Music

[hariri | hariri chanzo]

Bendi hiyo inaundwa na wasanii wafuatao:

  • Pius Polland – Mwandishi na mwimbaji
  • Yusuph Shitindi – Mwimbaji na mpiga ngoma
  • Mkapa Shiga – Mpiga gitaa la risasi na mwimbaji
  • Yohana Mwalyego – Mpiga besi / babatoni

Muziki na umaarufu

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2025, Hisili Music walitoa EP yenye nyimbo tano iliyopewa jina Hisili Ngoma Yetu. EP hii inajumuisha nyimbo maarufu kama:

Hata hivyo, Hisili Music wamewahi kutoa nyimbo nyingine ambazo zilifanya vizuri kama Nasema na Wewe na Kipepeo, ambazo pia zimepokewa vyema na mashabiki.

EP hii inapatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki ikiwemo Apple Music, YouTube, Boomplay na Audiomack.

Mwaka 2025, waliendelea kukuza muziki wao na kuimarisha uwepo wao kwenye majukwaa ya kidijiti.

Bendi hii imejizolea mashabiki wengi kupitia mitandao ya kijamii, ikiwa na zaidi ya 100,000 wafuasi kwenye TikTok na zaidi ya 1,000,000 watazamaji kwenye YouTube.

Mchango kwa Jamii

[hariri | hariri chanzo]

Hisili Music inavutia sana mtaani kutokana na nyimbo zao zinazogusa hisia, kuelimisha jamii, na kuonyesha maelewano ya karibu pamoja na umaridadi wao katika muziki.