Nenda kwa yaliyomo

Mbuga za Taifa la Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa mbuga za taifa nchini Tanzania.
Mahali pa mbuga za taifa nchini Tanzania.

Mbuga za Taifa za Tanzania[1] ni nyingi tena mbalimbali, zikishika karibu theluthi moja ya eneo lote la nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Zinagawanyika kati ya:

  • Hifadhi za Taifa,
  • Hifadhi Teule,
  • Hifadhi ya Mawindo na
  • Mapori ya Akiba.

Hifadhi za taifa

[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya Hifadhi za Taifa, ambazo ni 19:

Hifadhi za Taifa Kiingereza Mkoa
Hifadhi ya ArushaArusha NPArusha
Hifadhi ya Burigi-ChatoBurigi-Chato NPKagera, Geita
Hifadhi ya GombeGombe Stream NPKigoma
Hifadhi ya Ibanda-KyerwaIbanda-Kyerwa NPKagera
Hifadhi ya KataviKatavi NPSimiyu
Hifadhi ya kisiwa cha RubondoRubondo Island NPMwanza
Hifadhi ya kisiwa cha SaananeSaanane Island NPMwanza
Hifadhi ya KituloKitulo Plateau NPNjombe
Hifadhi ya MikumiMikumi NPMorogoro
Hifadhi ya Mlima KilimanjaroMount Kilimanjaro NPKilimanjaro
Hifadhi ya Milima ya MahaleMahale Mountains NPKigoma
Hifadhi ya Milima ya UdzungwaUdzungwa Mountains NPIringa, Morogoro
Hifadhi ya MkomaziMkomazi NPKilimanjaro, Tanga
Hifadhi ya RuahaRuaha NPIringa
Hifadhi ya Rumanyika-KaragweRumanyika-Karagwe NPKagera
Hifadhi ya SaadaniSaadani NPPwani
Hifadhi ya SerengetiSerengeti NPMara
Hifadhi ya TarangireTarangire NPManyara
Hifadhi ya Ziwa ManyaraLake Manyara NPManyara

Hakuna budi kuweka ulinzi mbugani kwani kuna majangili wanaoua ovyo wanyama kama vile tembo na kifaru: wanyama hao wanaweza kusaidia katika kuinua pato la taifa kupitia utalii.

Hifadhi za bahari na maeneo tengefu

[hariri | hariri chanzo]

Ni mpango wa kimataifa kuwa asilimia 10 ya maji ya bahari na maziwa yawe chini ya hifadhi, na Tanzania ina asilimia 4.5 tu ya hifadhi ambayo inahusisha hifadhi za bahari 3 na maeneo tengefu 15.

Hifadhi za bahari

[hariri | hariri chanzo]
Hifadhi ya kisiwa cha Mbudya, Dar es Salaam.

Hifadhi ya Bahari ni eneo kubwa ambalo hata watu wanaishi ndani yake. Shughuli za eneo hilo husimamiwa na Mpango wa Usimamiaji ujulikanao kama General Management Plan, ambao maandalizi yake yanashirikisha wadau woteː wanaoishi ndani ya hifadhi, Halmashauri husika ambazo ziko ndani ya hifadhi, na wengineo wakiwa ni pamoja na wanasayansi. Yanafanyika makubaliano ya kuwa baadhi ya maeneo yatengwe kabisa ambapo hakuna uvuvi wowote utakaoruhusiwa, kutenga maeneo ya matumizi ya jumla ambapo uvuvi unaruhusiwa kwa wavuvi wa ndani na nje ya hifadhi na maeneo ya matumizi maalum ambayo pamoja na kwamba wavuvi wa ndani ya hifadhi wanaruhusiwa kuvua kwa kutumia zana maalumu zinazokubalika, wavuvi wa nje hawaruhusiwi kabisa kuvua katika maeneo hayo.

Maeneo tengefu

[hariri | hariri chanzo]
Kisiwa cha Bongoyo

Maeneo tengefu ni maeneo madogomadogo ya visiwa ambayo yanazungukwa na matumbawe. Katika maeneo hayo watu hawaruhusiwi kuishi wala matumizi ya rasilimali hayaruhusiwi. Shughuli zinazoruhusiwa katika maeneo hayo ni zile zinazohusiana na utalii tu. Maeneo hayo ni pamoja na visiwa vya Bongoyo na Mbudya mjini Dar es Salaam ambapo ndani yake kitengo kimetengeneza njia vinjari (nature trails) kwa ajili ya watalii kupita.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: