Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Wanyamapori ya Okapi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Misitu ya Ituri kwa macho ya ndege
Okapi
Eneo la upatikanaji wa Okapi, pamoja na Hifadhi ya Okapi

Hifadhi ya Wanyamapori ya Okapi ni eneo katika msitu wa Ituri kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, karibu na mipaka na Sudan Kusini na Uganda. Eneo lake ni takriban km² 14,000, ikiwa na theluthi moja ya maeneo ya msitu wa Ituri. Inapitiwa na mito ya Nepoko, Ituri, na Epulu.

Hifadhi hii imepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia [1].

Hifadhi hiyo ilianzishwa hasa kwa ajili ya Okapi ambao ni wanyama wanaopatikana katika misitu ya Kongo pekee.

Hifadhi imekadiriwa kuwa makao ya okapi 5,000, tembo 4,000, chui 2,000, halafu sokwe mtu, na mamba. Wanyama wengine wa msitu wa Ituri ni pamoja na nyati. Hifadhi hiyo ina spishi zaidi ya 300 za ndege, ikiwa ni mojawapo ya maeneo muhimu kwa uhifadhi wa ndege katika Bara la Afrika. [2] Watu wanaoishi mle ni Wambuti ambao ni wafugaji wabilikimo, na wakulima Wabantu wa makabila mbalimbali.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi ya Wanyamapori ya Okapi ilianzishwa mnamo mwaka 1992. Changamoto kubwa ilikuwa kutunza hifadhi katika mazingira ya umaskini mkali na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Hatari kuu ni uenezaji wa ukulima wa kufyeka kwa msitu na uwindaji haramu wa wafanybiashara ya nyama ya pori, pamoja na uchimbaji wa dhahabu.

Mwaka 2005 mapigano ya vita ya wenyewe kwa wenyewe yaliingia ndani ya hifadhi ambako walinzi walipaswa kukimbia. Kituo cha kufuga okapi ndani ya hifadhi kilishambuliwa na wanamgambo wa Mai-Mai waliongozana na wawindaji wa tembo na wachimbaji haramu. [3] Okapi 14, wanyamapori mbalimbali na watu 6 waliuawa. Watu wengine wengi, pamoja na watoto, walitekwa nyara, lakini wote waliachiliwa baadaye. [4] Shambulio lilitokea tena mwaka 2017 ilhali wafanyakazi 6 waliuawa.

Mnamo 14 Julai 2017, kulikuwa na shambulio katika sehemu ya hifadhi karibu na Mambasa, labda la waasi wa Mai-Mai. Waandishi wa habari wa kigeni (wawili wa Uingereza na Mmarekani) na wasafiri kadhaa wa mbuga hiyo walitoroka bila kujeruhiwa, lakini wafanyakazi watano wa hifadhi wenyeji (watendaji wanne na tracker) waliuawa[5] [6].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "21 World Heritage Sites you have probably never heard of". Daily Telegraph.
  2. "Okapi Wildlife Reserve". Guide for Africa. Iliwekwa mnamo 2011-10-25.
  3. Okapi Conservation Project (28 June 2012).Okapi Conservation Project, Epulu Update – June 28, 2012 (https://web.archive.org/web/20120904160518/http://www.okapiconservation.org/news/okapi-conservation-project-epulu-update-june-28-2012/%7Cdate=September 4, 2012). Retrieved 15 September 2012
  4. Mongobay (9 September 2013).A year after devastating attack, security returns to the Okapi Wildlife Reserve (photos). Retrieved 16 July 2017.
  5. New York Times (16 July 2017).U.S. journalist found alive in Congo, 5 others are killed Archived 16 Julai 2017 at the Wayback Machine.. Retrieved 16 July 2017.
  6. France24 (16 July 2017).Kidnapped US journalist in DR Congo found safe, five wardens killed (https://web.archive.org/web/20170716155619/http://www.france24.com/en/20170716-kidnapped-us-journalist-dr-congo-okapi%7Cdate%3D2017-07-16%29. Retrieved 16 July 2017.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Wanyamapori ya Okapi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.