Hifadhi ya Taifa ya Bui

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya Mto unaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Bui
Sehemu ya Mto unaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Bui

Hifadhi ya Taifa ya Bui, inapatikana nchini Ghana ilianzishwa mnamo 1971. Eneo ni kilomita za mraba 1821. [1] Iko katika eneo la savana ya misitu. [2]

Hifadhi hiyo inajulikana kwa idadi kubwa ya viboko katika Volta Nyeusi. Tumbili aina ya colobus weusi na weupe na aina mbalimbali za swala na ndege wapo pia . [3] Sehemu ya hifadhi hiyo imefunikwa na hifadhi ya Bwawa la Bui, ambalo lilijengwa mnamo 2007 hadi 2013. [4]

Mahali[hariri | hariri chanzo]

Mbuga ya Taifa ya Bui imegawanywa na Mto Volta ; sehemu ya Magharibi ya mto ni sehemu ya eneo la Bono na sehemu ya Mashariki ya mto ni sehemu ya Mkoa wa Savannah wa Ghana . Hifadhi hiyo inapakana na Ivory Coast upande wa Magharibi. Miji ya karibu zaidi na hifadhi ni Nsawkaw, Wenchi na Techiman . [5] [6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. protected planet: Bui in Ghana Archived 12 Machi 2018 at the Wayback Machine.
  2. "Bui National Park, Ghana". www.oldwebsite.fcghana.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-01. 
  3. The Forest Commission of Ghana: Bui National Park, retrieved on May 7, 2011
  4. "Home". BUIPOWER (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-12-13. 
  5. "Bui National Park". Ghana Wildlife Division. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 February 2020. Iliwekwa mnamo 23 April 2018.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  6. WhiteOrange. "Brong Ahafo". Ghana Tourism Authority (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-06. Iliwekwa mnamo 2020-01-31.