Hifadhi ya Manovo-Gounda St. Floris

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Manovo-Gounda St. Floris National Park
MahaliCentral African Republic
Eneo17,400 km²
Kuanzishwa1979

Hifadhi ya Manovo-Gounda St. Floris ni mbuga ya kitaifa iliyopo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka wa Chad.

Ilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO mnamo 1988 kutokana na wingi wa bioanwai iliyomo ndani yake. Spishi zinazojulikana kuwamo ni pamoja na vifaru weusi, ndovu, Duma wa Sudani, Chui, Twiga, Nyati na Simba.

Hifadhi hii inatishiwa na uwindaji haramu.

Vifaru weusi wa magharibi ambao walikuwa wanyama asilia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wameshakoma mnamo 2011. Mnamo 1976 idadi ya Tembo ilikadiriwa kuwa kati ya 80,000 hadi 100,000, na mnamo mwaka 1985 walibaki kati ya 10,000 hadi 15,000 pekee. Tangu siku zile namba zimepungua tena ambapo mnamo mwaka 2005 ni Tembo chini ya 500 waliotazamwa kwa kutumia picha zilizochukuliwa kwa kutumia eropleni.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Manovo-Gounda St. Floris kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.