Hidrografia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa ramani inayoonyesha kina cha maji

Hidrografia (ing.hydrography) ni tawi la jiografia linalohusika upimaji wa magimba ya maji duniani kama vile bahari, maziwa na mito na tabia zao [1]. Neno hidrografia latokana na maneno ya Kigiriki ὕδωρ (hidor), "maji" na γράφω (grafō), "andika".

Kusudi muhimu ya kukusanya elimu hii ni usalama wa usafiri wa baharini na shughuli nyingine zinazohusika bahari na magimba ya maji mengine ya kimataifa kama matumizi ya kiuchumi, kijeshi, usalama, utafiti wa kisayansi na hifadhi ya mazingira. [2]

Shirika na taasisi mbalimbali za hidrografia zinakusanya data na kutoa ramani zimazoonyesha kina cha maji na njia za usafiri kwa maji kwa jumla kwa kusaidia usalama wa meli.[3]

Habari hii zilikusanywa tangu kale na kuoneshwa kwenye ramani zenye ilani kuhusu maeneo ambako kina cha maji kilikuwa kidogo na kudokeza kuwepo kwa miamba chini ya maji au mikondo katika maji zinazoweza kuhatarisha vyombo vya usafiri. Zamani habari hizi zilitunzwa mara nyingi kama siri kwa kusudi la kupata faida dhidi ya wafanyabiashara wengine au mataifa mengine.

Tangu kuongezeka kwa usafiri kwa maji pamoja na vyombo vya usafiri wakati wa karne ya 19 habari hizi zimesanifishwa zaidi na zaidi na kutolewa kwa umma kwa njia ya ramani zilizochapishwa.

Kuna taasisi nyingi za kitaifa zinazoshirikiana katika Shirika la Kimataifa la Hidrografia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]