Herbert Wimmer
| Herbert Wimmer | |
Wimmer mwaka 1972 | |
| Amezaliwa | 9 Novemba 1944 Eupen, Ubelgiji |
|---|---|
| Urefu | 1.79 m |
Herbert "Hacki" Wimmer (alizaliwa 9 Novemba 1944) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchini Ujerumani aliyecheza nafasi ya kiungo. Zaidi ya kushinda ubingwa wa kitaifa mara tano na kikombe cha UEFA mara mbili akiwa na klabu yake ya Borussia Mönchengladbach, alishinda Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 1974 na ubingwa wa mpira wa miguu wa ulaya wa mwaka 1972 akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani.
Taaluma ya klabu
[hariri | hariri chanzo]Wimmer alianza taaluma yake ya soka katika klabu ndogo ya Borussia Brand (eneo lililopo karibu na mji wa Aachen) huko nchini Ujerumani. Kati ya mwaka 1966 na 1978, alicheza mechi 366 za Bundesliga akiwa na Borussia Mönchengladbach na kufunga mabao 51.[1] Akiwa na klabu hiyo, alishinda ubingwa wa nchi mara tano (mnamo 1970, 1971, 1975, 1976, na 1977), Kikombe cha Ujerumani mnamo 1973, na kikombe cha UEFA mnamo 1975.
Wimmer alianza kama mshambuliaji, lakini akiwa Mönchengladbach, jukumu lake kuu lilikuwa kulinda safu ya ulinzi kwa ajili ya nyota wa timu katika enzi hiyo, kiungo mchezeshaji Günter Netzer. Uvumilivu wake wa kimwili, uliomfanya apewe jina la utani la "Iron Lung" (Pafu la Chuma), ulikuwa mmoja wa uwezo wake mkubwa. Wimmer alichukuliwa kuwa mfano wa mchezaji asiyechoka kabisa. Kutokana na hilo, mwandishi Jonathan Wilson, akiandika katika jarida la "The Guardian mnamo mwaka 2013, alimweleza kama "mharibu" (destroyer), ambalo ni aina ya kiungo mkabaji ambaye jukumu lake kuu ni kusaidia kurejesha mpira na kuusambaza kwa wachezaji wengine.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Arnhold, Matthias (3 Machi 2022). "Herbert Wimmer - Matches and Goals in Bundesliga". RSSSF.com. Iliwekwa mnamo 3 Machi 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wilson, Jonathan (18 Desemba 2013). "The Question: what does the changing role of holding midfielders tell us?". The Guardian. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Herbert Wimmer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |