Henrie Mutuku
Henrie Mutuku |
---|
Henrie Mutuku ni mwanamuziki wa Injili kutoka nchini Kenya ambaye ameshinda tuzo nyingi.
Maisha ya utotoni
[hariri | hariri chanzo]Mutuku alizaliwa mjini Nairobi mwaka 1978, mzaliwa wa kwanza na ndugu watatu kwa wazazi wao. Alikulia katika eneo la Eastlands, eneo ambalo linakaliwa na watu wengi wenye mapato ya chini katika mji wa Nairobi, na alipata kuaona mitindo mbalimbali ya muziki akiwa na umri mdogo sana kama vile R & B, Reggae, Rap, Benga, Kilingala na nyingine za Afrika.
Alijifunza kuimba na kucheza piano, na kuanza kutumbuiza mapema katika kongamano za familia kabla ya kufuzu kwa kuimba katika Sunday School katika kanisa jirani na baadaye katika kwaya ya kanisa. Mutuku alifikiriw kushughulika na wasifu kuimba wakati wa shule ya upili, ambapo alikuwa ni mwanachama hai wa Kilabu cha Uigizaji na Mkuu wa Kwaya ya shule.
Yeye huongea lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kamba (lugha ya mama) na Sheng.[1]
Wasifu wa muziki
[hariri | hariri chanzo]Henrie ilianza kazi katika muziki pamoja na wasanii wa Kikristo mitaani kama vile Izzo na Pete Odera kama muimbaji wa nyuma. Baadaye alijihusisha kwa sana katika mkusanyiko wa albamu ya mwaka 2002 'Rebirth' iliyotayarishwa na Soul Child Inc [2]. Uimbaji wake uliimarika baada ya kushinda tuzo mbili za Msanii Bora wa Afrika Mashariki za Kora mwaka wa 2002 .[3]
Albamu yake ya kwanza ilikuwa "Simama" (Stand) ambayo nyimbo kama "Usichoke" (akimshirikisha Roughtone na RK) na "Manzi wa Maana" (akimshirikisha KJ wa Redykulass-aKundi la waigazaji wacheshi la Kenyan). Pia amemshirikishwa katika vipindi vya redio katika vituo vya redio kadhaa maarufu kama Kiss 100 “Smirnoff Top 7 songs in Nairobi”, East Africa FM Radio ‘Link’ na Kampala FM as voted by listeners.
Mutuku amemfungulia pazia Bebo Norman kwenye matamasha mbili , na kumfanya kurekodi video yake ya kwanza ya muziki, "Nakuhitaji" (I Need you), iliyotayarishwa na televishani ya kimtaa ya Family TV kwa ajili ya uendelezaji wa Bebo Norman Tour. Hiuvi karibuni ametoa video ya wimbo wa "Amini" (Believe), ni mojawapo katika albamu yake ya 'Simama'.
Mwaka wa 2003 alishinda tuzo mbili katika 2Tuzo za Kisima kama Msanii Bora wa Kike Msanii Bora wa Kike wa muziki wa Injili ya Kisasa [4] Pia alitajwa kushiriki kwenye Tuzo za Kora za mwaka wa 2003 [5]
Mutuku hushiriki kikamilifu katika shughuli za uchangishaji fedha na shughuli za kuzuia UKIMWI, watoto yatima na wagonjwa wa UKIMWI, Protecting Life Movement nchini Kenya na tafsiri ya Biblia na kusoma.
Angalia Pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti Rasmi Archived 26 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Official Biography". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-09. Iliwekwa mnamo 2010-01-17.
- ↑ Chorus of hope as 8 Kenyans enter fete, by Njoki Karuoya, published on Saturday Nation on the Web [1]
- ↑ Henrie and Eric strike a chord for Kenya, by Amos Ngaira, published on Daily Nation on the Web [2]
- ↑ "Kisima Music Awards - 2003 Winners". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-08-07. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
- ↑ Tuzo za Kora: Wateule 2003
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Henrie Mutuku kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |