Henri Morse

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Henri Morse.

Henri Morse, S.J. (Brome, Suffolk, Uingereza, 1595Tyburn, London, 1 Februari 1645) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki ambaye alifukuzwa nchini na mfalme mara mbili, lakini akarudi kufanya uchungaji hadi alipofungwa gerezani na, baada ya kuadhimisha Misa, aliuawa kikatili na serikali ya Uingereza.

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929 halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[1].

Sikukuu yake ni tarehe 1 Februari[2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Henri alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki nchini Ufaransa alipomfuata ndugu yake Wiliamu aliyekuwa seminarini.

Baada ya kurudi Uingereza, alifungwa miaka minne kwa imani yake mpya, halafu akaweza kurudi bara kwa kengo la kupata upadrisho na hatimaye kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali ya nchi yake.

Baada ya kupadrishwa Roma alirudi kwao (1624) na tauni ilipozuka alihudumia waathirika huko Newcastle-upon-Tyne halafu York Castle. Katikati alifungwa halafu akajiunga na Wajesuiti. Baada ya miaka mitatu gerezani aliachiwa na kufukuzwa nchini, hivyo akafanya uchungaji Uholanzi.

Mwaka 1633 alirudi Uingereza akapatwa na tauni katika kuhudumia tena waathirika, akapona. Mwaka 1636 akakamatwa tena kwa imani yake lakini aliachiwa mwaka uliofuata akahama nchi kwa muda hadi mwaka 1643. Baada ya kufanya utume wake Uingereza kwa mwaka mmoja na nusu tena aliuawa kwa kuchanwachanwa kikatili chini ya sheria.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Malcolm Pullan (30 April 2008). The Lives and Times of Forty Martyrs of England and Wales 1535 - 1680. Athena Press. pp. xvii–xxiai. ISBN 978-1-84748-258-7.
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.