Nenda kwa yaliyomo

Helena wa Troia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Helen wa Troy)
Helen wa Troy na Evelyn de Morgan (1898, London).

Helena wa Troia alikuwa malkia wa Sparta aliyetekwa nyara na kupelekwa Troia, tendo lilioanzisha Vita ya Troia inayosimuliwa katika Utenzi wa Iliadi wa Homer.

Katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale, Helena alikuwa mtoto wa malkia Leda wa Sparta na mungu mkuu Zeu. Alisemekana alikuwa mzuri kushinda wanawake wote duniani.

Helena aliolewa na Menelao aliyeendelea kuwa mfalme wa Sparta. Baadaye alitoroka na kijana Paris wa Troia, mtoto wa mfalme Priamo, wengine walisema alitekwa nyara naye.

Majaribio ya kumrudisha Sparta yalisababisha vita ya Troia.

Mapokeo ya Wagiriki wa Kale hitofautiana kuhusu maisha yake; katika umbo linalojulikana zaidi, yaani masimulizi ya Homer, alipelekwa Troia alipokaa hadi mwisho wa vita; mume wake Menelao alimsamehe wakarudi pamoja Sparta walipoishi miaka mingi kwa furaha.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: