Nenda kwa yaliyomo

Hashim Thabit Manka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hasheem Thabeet mwaka 2010.

Hasheem Thabeet (jina kamili: Hashim Thabit Manka; alizaliwa Dar es Salaam, 16 Februari 1987) ni mchezaji wa mpira wa kikapu kutokea Tanzania anayeichezea timu ya Fort Wayne Mad Ants katika Chama cha taifa cha mpira wa kikapu (NBA) ligi G. [1]Alichaguliwa kama chaguo la pili baada ya kutofanya vizuri [2]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Hashim Thabit alianza kucheza kwa kujitolea mpira wa kikapu akiwa na miaka 15, alipochukuliwa kutoka Tanzania Hasheem alikuwa akizungumza kiswahili fasaha Swahilialiongea kimombo kiasi .[3] Aliendelea kuchezea timu yake ya shule ya upili ya Cypress Christian School in Houston, Texas baada ya kuhitimu mwaka 2006.

Akiwa mwanafunzi mpya katika chuo cha Connecticut Huskies aliweza kufikia wastani wa alama 6.2 na alama za kuzuia 3.8 kwenye mchezo mmoja . [4] Tarehe 3 Desemba mwaka 2006,Hashim aliweka rekodi ya kuzuia kwenye mchezo mmoja kwa kufikisha point 10 akiwa na timu yake ya UConn[5] na mchezaji mwenzie Jerome Dyson.

Alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili chuoni ,aliweza kufikisha wastani alama 10.5, na alama 7.9 kwa mipira ya kurudisha na alama 4.5 za kuzuia katika msimu mmoja. [4] Tarehe 5 Januari 2008, aliendelea kufanya vizuri na timu yake ya Huskies kwa kufikisha kuzuia mara 10 kwenye mchezo waliopoteza kwa alama' 73–67 katika University of Notre Dame.[6]Hashim alipewa tuzo ya mchezaji bora anayechezea nafasi ya kuzuia wa mashariki, kwenye timu ya pili ya wakubwa ya mashariki

Akiwa bado ana umri mdogo ,Hashim alionekana kitaifa baada ya kufikisha wastani wa alama 13.6 na alama 10.8 ya mipira ya kurudisha.Alianza kujikita zaidi kwenye mchezo huo triple-double akilipocheza dhidi ya Providence College tarehe 31 Januari Mwaka 2009 akipata alama 15 na 11 mipira ya kurudisha na kuzuia mara 10 [7] Alizuia mara 152 msimu mzima. Alitajwa kuwa mchezaji bora wa kuzuia mashariki ya wakubwa Big East Player of the Year with Pitt's DeJuan Blair.[8].Hashim alitajwa kuwa mchezaji wa timu ya pili kitaifa ya mchezaji bora wa kuzuia kitaifa. Hashim alipita alama 1000 dhidi ya Purdue alikuwa mcheza wa tatu wa UConn kufikia rekodi kwenye msimu huo (Jerome Dyson na A. J. Price ndio wachezaji wengine walioweza kufikia hiyo rekodi).Hashim aliisaidia timu yake ya UConn kwa mara ya kwanza kufika kwenye finali za t Final Four mwaka 2004 Akiwa mwaka mwaka wake wa mwisho chuo, Hashim alichaguliwa na chama kinachosimamia ligi ya mpira wa kikapu kitaifa cha NBA kama mmoja ya wa chezaji wanaoruhusiwa kuchezea ligi hiyo

Hasheem alichezea timu ya chuo cha UConn kabla ya kuchaguliwa kama chaguo la pili mwaka 2009 katika timu ya Memphis Grizzlies.

Urefu wake ni mita 2.21.

  1. "Hasheem Thabeet NBA & ABA Stats". Basketball-Reference.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-07. Iliwekwa mnamo 19 Novemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Spears, Marc J. (Novemba 16, 2016). "NBA or bust: Hasheem Thabeet refuses to give up on going back to the league". The Undefeated. Iliwekwa mnamo Novemba 25, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Biggest Man on Campus – Tanzanian freshman tallest ever at UConn", SI.com, 18 July 2006. Retrieved on 29 October 2009. Archived from the original on 9 September 2009. 
  4. 4.0 4.1 "Hasheem Thabeet College Stats - College Basketball at Sports-Reference.com". College Basketball at Sports-Reference.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-10. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Thabeet's record 10 blocks key UConn's big win – College basketball – MSNBC.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-29. Iliwekwa mnamo 2020-02-01.
  6. "Connecticut vs. Notre Dame - Game Recap - January 5, 2008 - ESPN". ESPN.com. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Providence vs. Connecticut - Game Recap - January 31, 2009 - ESPN". ESPN.com. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Blair, Thabeet share Big East award". Iliwekwa mnamo 19 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hashim Thabit Manka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.