Nenda kwa yaliyomo

Harriet Margaret Louisa Bolus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Harriet Margaret Louisa Bolus née Kensit (31 Julai 1877 huko Burgersdorp - 5 Aprili 1970 huko Cape Town) alikuwa mtaalamu wa mimea na uainishaji wa mimea wa Afrika Kusini, na mhifadhi wa kipindi kirefu wa Bolus Herbarium, kuanzia mwaka wa 1903. Bolus pia ana historia wa kuandika spishi nyingi zaidi za mimea ya ardhini kuliko mwanasayansi mwingine yeyote wa jinsia ya kike, kwa jumla akitaja spishi 1,494. [1]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Bolus alizaliwa mahali panaitwa Burgersdorp, Jimbo la Rasi, Afrika Kusini, tarehe 31 Julai 1877. Alikuwa binti wa William Kensit na Jane Stuart Kensit. Wazazi wake wote walizaliwa Uingereza. [2] Babu yake William Kensit alikuwa mtaalamu wa mimea na mkusanyaji sampuli nchini Afrika Kusini. Alipata elimu kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vyuo Vikuu huko Port Elizabeth, akapata sifa ya ualimu mnamo 1899, na akatunukiwa shahada ya BA kwenye fasihi na falsafa na Chuo Kikuu cha Cape of Good Hope mwaka mnamo wa 1902. [3]

Alifanya kazi kwa nafasi ya msaidizi wa mume wa shangazi yake mkubwa Sophia, Harry Bolus, kwenye bustani yake ya mimea alipokuwa chuoni. Kipindi cha Juni 1913, akawa mwanachama mwanzilishi wa baraza la Jumuiya ya Mimea ya Afrika Kusini; pamoja na kuwa mwanachama mwanzilishi wa Jumuiya ya Ulinzi wa Maisha ya Wanyamapori, na mwanachama wa Jumuiya ya Kifalme ya Afrika Kusini, Jumuiya ya Linnean, na Chama cha Kusini mwa Afrika cha Maendeleo ya Sayansi . [2] Alichaguliwa kuwa msimamizi wa Bolus Herbarium mwaka wa 1903, na akastaafu kutoka nafasi hiyo mwaka 1955. [4] Alimwajiri msanii wa mimea Louise Guthrie kama mfanyakazi katika bustani hiyo ya mimea. [5]

Kitabu chake cha kwanza, Masomo ya Msingi katika Botania ya Kimfumo, kilichapishwa mwaka wa 1919. [2] Hiki kilifuatiwa na vitabu viwili vinavyohusu maua ya Afrika Kusini. [6] [7] Louisa alitoa michango kwenye majarida kadhaa ya mimea katika maisha yake yote, na akahariri Annals of the Bolus Herbarium . [8]

Louisa Bolus alimimina muda mwingi wa maisha yake akiendekeza utafiti wa kina juu ya Mesembryanthemum . Maelezo yake juu ya Mesembryanthemum na Allied Genera yalichapishwa mnamo wa 1927. [9] Hii ilifuatiwa na uchapishaji wa vitabu vitatu, vinavyoelezea maelezo ya kina ya Kilatini ya takriban mimea 1500. Mwaka wa 1936 Louisa alipewa shahada ya heshima ya Uzamivu wa Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch . [10]

Mmea unaotokana na familia kubwa ya Mesembreyanthemum, jenasi Kensitia ulirasimishwa kwa lengo la kuheshimu kazi ya Bolus juu ya mada hii. Louisa Bolus alichangisha mchango wake kwa Flowering Plants of South Africa, iliyohaririwa na EP Phillips mnamo 1943, na mwaka wa 1951 akashika nafasi ya mdhamini wa uchapishaji wa Wild Flowers of the Cape of Good Hope na Elsie Garrett Rice na RH Compton . Bolus pia alichukuliwa kuwa mwanzilishi wa madarasa ya masomo ya asili katika Bustani ya Kitaifa ya Mimea ya Kirstenbosch . [2] Mwaka wa 1966, akawa makamu wa rais wa Jumuiya ya Mimea ya Succulent ya Afrika.

Bolus alipata elimu juu ya mimea ya eneo linalozunguka Cape of Good Hope, hasa juu ya Ericaceae na juu ya Orchidaceae . Alichapisha mara nyingi kwenye majarida ya mimea pamoja na makala na vitabu maarufu vya bustani, hasa Kitabu cha Mimea ya Afrika Kusini . Aliteuliwa kuwa Mwanachama wa Jumuiya ya Kifalme ya Afrika Kusini mwaka wa 1920 na akapokea udaktari wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch . Jenasi Bolusanthus na spishi Geissorhiza louisabolusiae zimepewa jina kwa heshima yake. [3]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1912 Louisa aliolewa na mwana wa Harry Bolus (na binamu wa baba yake) Frank Bolus. Alikuwa mjane kipindi Frank Bolus alipofariki dunia mwaka wa 1945. Louisa Bolus alifariki nyumbani kwake huko Claremont, Cape Town mwaka wa 1970 akiwa na umri wa miaka 93. [2]

  1. Lindon et al. 2015.
  2. 1 2 3 4 5 Creese & Creese 2010.
  3. 1 2 Ogilvie & Harvey 2000.
  4. Staples.
  5. Rourke 2001.
  6. Bolus & Barclay 1928.
  7. Bolus 1936.
  8. Bolus 1914.
  9. Bolus 1927.
  10. Gunn & Codd 1981.