Nenda kwa yaliyomo

Hands On (mfululizo wa TV)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hands On ni kipindi cha televisheni kwa ajili ya viziwi na watu wenye usikivu hafifu nchini Ayalandi. Kipindi hiki hurushwa siku ya Jumapili, mara mbili kwa mwezi kupitia RTÉ One[1] Chaneli ya kituo cha taifa cha utangazaji wa umma nchini Ayalandi. Kipindi cha Hands On kilianza kurushwa kwenye RTÉ mwaka 1996, kikichukua nafasi ya kipindi kilichotangulia kiitwacho Sign of the Times, ambacho kilionyeshwa kati ya 1988 hadi 1995.

Hands On hurushwa hewani na timu yenye watangazaji tisa mchanganyiko wa viziwi na watu wanaosikia. Wanawasilisha kipindi kwa kutumia Lugha ya Alama ya Ayalandi (ISL), ambayo ni lugha ya kwanza ya jamii ya viziwi nchini humo. Kipindi pia huwa na maandishi ya maneno yanayotembea na sauti ya Kiingereza kwa wale wasiotumia lugha ya alama. [2] [3]

  1. https://tv.signlangtv.org/shows/rte-hands-on/
  2. https://www.imdb.com/title/tt1647675/episodes/?season=18
  3. https://tv.signlangtv.org/shows/mode/deaf-presented/