Nenda kwa yaliyomo

Hana Elhebshi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hana Elhebshi

Nchi Libya
Kazi yake Mwanaharakati na mbunifu wa majengo

Hana Elhebshi (Kiarabu: هناء الحبشي; alizaliwa takribani mwaka 1985) ni mwanaharakati na mbunifu wa majengo (architect) kutoka Libya.[1]

Elhebshi alifanya kazi kama mbunifu wa majengo mjini Tripoli. Baba yake alikuwa kamanda wa kijeshi aliyekuwa akiendesha Jeshi la Anga katika kambi ya Noviaga Aligeuka kuwa mwanaharakati wakati wa Mapinduzi ya Libya, licha ya kwamba kabla ya hapo hakuwa akijihusisha na siasa. [2]Alikuwa mwanaharakati wa mtandaoni (cyberactivist), akiripoti mtandaoni kuhusu kuzingirwa kwa Tripoli.

Aliishauri NATO kuhusu mashambulizi yake na aliweka hadharani idadi ya watu waliouawa na utawala wa Muammar Gaddafi wakati wa Mapinduzi ya Libya. Pia alitaka kuzungumza ili kuieleza dunia mateso ambayo Libya ilikuwa imepitia kwa miaka mingi[3]

  1. "Libyan Activist Gets International Women of Courage Award". www.tripolipost.com. Iliwekwa mnamo 2026-01-10.
  2. "Pittsburgh first U.S. city to spend time with courageous women". Pittsburgh Post-Gazette (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-10.
  3. "2012 International Women of Courage Award Winners". www.state.gov. Iliwekwa mnamo 2026-01-10.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hana Elhebshi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.