Hamud bin Mohammed wa Zanzibar

Hamud bin Mohammed Al-Buwsaid (kwa Kiarabu: حمود بن محمد البوسعيد; 1853 hivi – 18 Julai 1902) alikuwa Sultani wa saba wa Zanzibar. Alitawala Zanzibar kuanzia tarehe 27 Agosti 1896 hadi kifo chake, aliporithiwa na mmoja kati ya watoto wake 10, Ali bin Hamud.
Hamud alirithi madaraka chini ya usimamizi wa Waingereza, kwa sababu Sultani Sayyid Hamad bin Thuwaini Al-Busaid alipofariki ghafla tarehe 25 Agosti 1896 saa 5:40 asubuhi, ikisemekana mara baada ya kupewa sumu na binamu yake Khalid bin Barghash, huyo alijitangaza kuwa sultani mpya. Khalid aliendelea kushikilia kiti cha enzi kwa siku tatu tu kabla ya kuondolewa na majeshi ya Waingereza katika vita vya Uingereza dhidi ya Zanzibar, vinavyotambulika kama vita vya muda mfupi kabisa katika historia ya dunia.[1].
Hamud alifuta utumwa visiwani na kudai watumwa waachiliwe, isipokuwa masuria[2].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hernon, Ian (2003). Britain's Forgotten Wars. Stroud: Sutton Publishing. ku. 396–404. ISBN 978-0-7509-3162-5.
- ↑ The End of Slavery in Africa. (1988). USA: University of Wisconsin Press. 23
| Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hamud bin Mohammed wa Zanzibar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |