Halkidiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Halkidiki katika Ugiriki

Halkidiki (pia: Chalkidiki; Kigir. Χαλκιδική) ni rasi ya Ugiriki ya kaskazini inayoingia katika bahari ya Mediteranea kwa umbo la mkono mwenye vidole vitatu. Kidole upande wa mashariki ni Athos inayojulikana kama jamhuri ya Wamonaki; ni kama jimbo la kujitegemea linalosimamiwa na Ugiriki kwa mambo ya nje tu.

Kihistoria Halkidiki ilikuwa sehemu ya Masedonia ya Kigiriki. Mwanafalsafa mashuhuri Aristoteli alizaliwa hapa.

Leo hii Halkidiki -isipokuwa sehemu ya Athos- ni moja kati ya wilaya 51 za Ugiriki na makao makuu iko mjini Polygyros.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Halkidiki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.