Hali ya hewa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 17:56, 19 Novemba 2013 na Kipala (majadiliano | michango)
Pinde ya mvua inaonyesha rangi nyingi ni alama ya kupendeza

Hali ya hewa (pia: halihewa) ni namna ya kutaja yale yanayotokea katika sehemu ya chini ya angahewa juu ya uso wa dunia katika eneo fulani na wakati fulani.

Hali hizi hutofautishwa kulingana na upepo, halijoto, umawingu, unyevuanga, kanieneo, mnururisho wa jua, uvukizaji na kadhalika.

Sayansi ya metorolojia huifanyia halihewa utafiti kwa kupima hali mbalimbali hadi kutabiri mabadiliko yanayokuja karibuni. Athari muhimu zaidi katika mabadiliko ya halihewa ni mzunguko wa angahewa unaotawaliwa na nishati ya mnururisho wa jua na uwiano wa kani katika eneo fulani.

Tabia muhimu za halihewa hutokea kama upepo, dhoruba, kimbunga, radi, mvua, theluji na baridi au joto zikiathiri maisha ya kibinadamu.

Hali ya hewa inaenda sambamba na tabianchi yaani kama ni ya joto au baridi, bichi au yabisi. Mabadiliko ya hali ya hewa hurahisihsa maisha au kuongeza ugumu hasa kama mabadiliko yanavurugisha kukua kwa mimea kwa njia ya ukame au mafuriko.

Watu hujenga makao na kuvaa nguo kulingana na halihewa na kwa njia hiyo tabianchi imekuwa nguvu ya kufinyanga utamaduni wa watu.

Hali ya hewa hutazamiwa tofauti katika tamaduni na nchi mbalimbali. Katika Afrika penye hatari ya ukame kwa kawaida mvua hutazamiwa kama baraka; lakini Ulaya penye mvua nyingi watu hufurahia jua na watoto wanaambiwa: "Usipomaliza chakula kwenye sahani yako mvua itanyesha" (msemo wa Kijerumani).


Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hali ya hewa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.