Nenda kwa yaliyomo

Haki ya kuwa na maji na mazingira salama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upatikanaji wa Maji

Haki ya kuwa na maji na mazingira salama ni mojawapo kati ya haki za binadamu inayohusu umuhimu wa maji safi na salama na usafi wa mazingira kwa maisha ya binadamu.

Haki hiyo ilitambuliwa na kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 28 Julai 2010. Pia, haki hiyo imetambuliwa katika sheria za kimataifa kupitia mikataba ya haki za binadamu na matamko mbalimbali ya kimataifa yanayohusu haki za binadamu.

Baadhi ya wahanga wa haki hiyo walitoa maoni yanayothibitisha kupatikana kwa haki hiyo baada tu ya azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutoka katika Kifungu cha 11.1 cha Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, na kuifanya kuwa ya lazima chini ya sheria za kimataifa katika nchi mbalimbali.[1]

  1. "International Decade for Action 'Water for Life' 2005-2015. Focus Areas: The human right to water and sanitation". United Nations (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-12.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Haki ya kuwa na maji na mazingira salama kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.