Haki ya Kidigitali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Haki ya Kidigitali (Kiingereza Digital Right) ni moja ya haki za binadamu na haki za asili na kisheria zinazomruhusu mtu au binadamu kuweza kutumia,kutengeneza pamoja na kuchapisha maudhui katika vyombo vya kidigitali ,au kuwa na uwezo na uhuru wa kutumia Kompyuta pamoja na vifaa vingine vya kielektronik na vifaa vya mawasiliano. Dhana ya uhuru wa Kidigitali inahusiana na ulinzi wa kidigitali na utambuzi wa haki za kidigitali zilizopo kama vile Haki ya Faragha na Uhuru wa Kujieleza, katika muktadha wa teknolojia ya kidigitali pamoja na intaneti[1] Nchi kadhaa duniani zimetambua na kupitisha Uhuru wa kuwa na uwezo wa kutumia Intaneti[2]

Haki za Binadamu na Intaneti[hariri | hariri chanzo]

Idadi kubwa ya haki za binadamu zimekuwa zikitambuliwa moja wapo ya haki hizo ni zile zinazohusiana na matumizi ya Intaneti, haki hizi za intaneti zinahusiana na na Uhuru wa Kujieleza, Haki ya Fragha, na uhuru wa Mashirikiano, pia, haki za kidigitali zinahusiana na Haki ya Elimu, lugha, Kujengeana Uwezo pamoja na Haki za Kimaendeleo[3][4]

Kulingana na jarida la La Civilta Catttolica katika makala yake linasema kuwa Intaneti ina faida na manufaa kwa umma na inapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa kama haki nyingine, serikali za kidemokrasia duniani zinapaswa kupitisha na kuwezesha sheria za matumizi ya intaneti pamoja na kupitisha sheria zitakazosimamia matumizi ya intaneti na haki za binadamu

Makala hiyo inaendelea kusema "Kile ambacho sheria inaruhusu nje ya mtandao basi kinafaa pia kuruhusiwa ndani ya mtandao,pia, masuala ya mtandaoni yanapaswa kuzingatia udhibiti wa Ugaidi wa Kimtandao pamoja na kulinda maudhui ya Ponoografia kwa watoto pamoja kupinga au kuzuia ubaguzi wa rangi,makala hiyo iliendelea kuelezea kuwa Dunia inahitaji Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu Kimtandao pamoja na kuwa watu wanaendelea kutumia vibaya mtandao huku makampuni ya Kompyuta na Intaneti yakiendelea kujipatia faida na kutengeneza pesa


Haki ya Kidigitali Nchini Tanzania[hariri | hariri chanzo]

Nchi nyingi duniani zimekuwa na sheria zake katika matumzi ya intaneti ikiwemo Tanzania ambayo inasheria mbalimbali za matumizi ya mtandao Taasisi na Asasi isiyo ya kiserikali mfano taasisi ya Zaina Foundation zimekuwa zikitoa mafunzo kuhusiana na matumzi ya intaneti na haki za kidigitali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Scale of justice 2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Haki ya Kidigitali kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.