Hajj Sayyah
Mirza Mohammad Ali, anajulikana zaidi kama Hajj Sayyah ( 91836–1925), alikuwa msafiri wa dunia na mwanaharakati wa kisiasa mwenye asili ya Uajemi na Marekani (Iranian American).
Alikuwa Mwirani wa kwanza kupata Uraia wa Marekani. Kulingana na amri iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Wilaya ya 12 ya Kimahakama ya Jimbo la California, alipewa uraia huo mnamo tarehe 26 Mei 1875.
Maisha ya mapema
[hariri | hariri chanzo]Hajj Sayyah alizaliwa mnamo mwaka 1836 katika mji wa Mahallat, Dola Kuu ya Iran.[1] Masomo yake katika umri mdogo yalimfanya afahamu mawazo ya kisasa na ya kidemokrasia ambayo wakati huo yalikuwa yakisambaa katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti kubwa alizoziona kati ya utawala wa kiimla nchini Iran na mawazo hayo aliyosomea zilimpa msukumo wa kwenda kuuona ulimwengu uliosalia.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Mehrbanoo Nasser Deyhim in: An Iranian in Nineteenth Century Europe, The Travel Diaries of Hâj Sayyâh 1859-1877. Translated by Mehrbanoo Nasser Deyhim, Foreword by Peter Avery. Bethesda Maryland, IBEX Publishers 1998. p.15.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hajj Sayyah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |