Haji Manara
Haji Sunday Manara alimaarufu Bugati (amezaliwa 18 Januari 1975) ni msemaji wa vilabu vya michezo, mwanahabari, mjasiriamali na mwanasiasa kutoka Tanzania. Anajulikana zaidi kwa nafasi zake kama msemaji wa vilabu vya soka vya Simba SC na Young Africans SC (Yanga SC), pamoja na mtindo wake wa kipekee wa mawasiliano ya michezo.[1]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Haji Manara alizaliwa Amsterdam, Uholanzi, na kukulia nchini Tanzania. Ni mtoto wa Sunday Manara, aliyekuwa mchezaji wa mpira Ulaya na Tanzania.[2] Alisoma elimu ya msingi katika shule za Mnazi Mmoja na Bunge zilizopo Dar es Salaam. Elimu yake ya sekondari aliipata Chimala Secondary School (Mbeya) kwa O-Level na Mzumbe Secondary School (Morogoro) kwa A-Level. Aidha, alipata elimu ya dini nchini Saudi Arabia na baadaye kusomea mawasiliano ya umma (Mass Communication) nchini Afrika Kusini.[3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Manara alianza kazi yake katika vyombo vya habari kama mtangazaji wa redio, akifanya kazi na Uhuru Radio. Pia aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya Index International.
Katika siasa, aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kati ya mwaka 2007 na 2010. Na ni diwani wa kata ya Kariakoo. [4]
Katika soka, alijizolea umaarufu mkubwa alipokuwa msemaji wa klabu ya Simba SC kuanzia mwaka 2015 hadi 2021. Baada ya kuondoka Simba SC mwaka 2021, alijiunga na klabu ya Young Africans SC (Yanga SC) kama msemaji rasmi.
Mbali na soka, Manara amefanya kazi kama balozi wa chapa mbalimbali ikiwa ni pamoja na GSM, Azam Media na Bayport. Pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Manara Media/Manara TV, na ametangaza mipango ya kuanzisha kituo cha redio.
Migogoro
[hariri | hariri chanzo]Katika maisha yake ya kazi, Manara amekumbwa na migogoro mbalimbali. Mwaka 2010 alikumbana na tuhuma za udanganyifu wa magari, lakini baadaye aliachiliwa.
Mwaka 2021 aliondoka Simba SC kufuatia mgogoro na uongozi wa klabu hiyo. Mwaka 2022 alifungiwa kwa muda wa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na kutozwa faini kutokana na masuala ya kinidhamu.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Haji Manara ni mtoto wa Sunday Manara, aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Young Africans SC. Anatoka katika familia yenye historia ya soka nchini Tanzania.
Katika maisha yake ya mahusiano, alihusishwa na muigizaji Zainab Saidi (maarufu kama Zaiylissa), ambaye walifunga ndoa mwaka 2024.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.mambodaily.com/2023/12/haji-manara-age-cv-and-bio.html
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/makala/spoti-mikiki/sunday-manara-kompyuta-mtanzania-wa-kwanza-ulaya-2782246
- ↑ https://clickhabari.com/ifahamu-historia-ya-haji-manara/
- ↑ https://kaziforums.com/haji-manara-umri-kuzaliwa-watoto-mke-nakadhalika/