Nabii Hagai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hagai)
Jump to navigation Jump to search
Picha ya Kirusi ya Hagai, karne ya 18 (katika ukuta wa picha wa monasteri ya Kizhi, Karelia, Russia).

Nabii Hagai (kwa Kiebrania חַגַּי, Ḥaggay au "Hag-i", yaani sikukuu yangu; kwa Kigiriki: Ἀγγαῖος; kwa Kilatini Aggeus) ni mmojawapo kati ya wa manabii wa Israeli, aliyefanya kazi miezi ya mwisho ya mwaka 520 KK tu, akihimiza pamoja na nabii Zekaria ujenzi mpya wa hekalu la Yerusalemu baada ya Wayahudi kurudi toka uhamisho wa Babeli.

Hatimaye kazi ilikamilika na hekalu likatabarukiwa mwaka 515 KK.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Kitabu chake ni kati ya Manabii Wadogo 12 wa Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), kwa hiyo pia kinapatikana katika Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Heshima baada ya kifo[hariri | hariri chanzo]

Hagai anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 16 Desemba au 29 Desemba au 31 Julai.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Carroll Stuhlmueller, Haggai and Zechariah: Rebuilding With Hope. Edinburgh: The Handsel Press Ltd., 1988. ISBN 978-0-905312-75-0.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]