Hadja Saran Daraba Kaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Hadja Saran Daraba Kaba
Nchi Guinea
Kazi yake Mwana harakati

Hadja Saran Daraba Kaba (alizaliwa 1945) ni mwanaharakati wa wanawake wa Guinea, Katibu mkuu wa kwanza mwanamke wa Umoja wa Mto Mano na mgombea uraisi wa 2010 kwenye uchaguzi mkuu wa Guinea. [1]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Hadja Saran Daraba Kaba alizaliwa 1945 kuelekea mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia huko Coyah, Guinea kwenye familia isiyo na uwezo, baba yake alikuwa mwanajeshi na mwanaharakati chini ya utawala wa Hayati Raisi Ahmed Sékou Touré . Alitengeneza silaha zake za kisiasa akiwa na umri mdogo. Alipata mafunzo kama mfamasia huko Leipzig na Halle nchini Ujerumani kati ya 1966 na 1979. Mnamo 1970, alirejea Guinea ambako alifundisha katika Kitivo cha tiba na Famasia cha Hadja Mafory Bangoura na baadaye akajiunga na Pharmaguinée ambako alipanda hadi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Kitaifa wa Mauzo ya Nje katika Wizara ya Biashara ya Nje. Mnamo 1996 alikua Waziri wa Masuala ya Jamii na Ukuzaji wa Wanawake na Watoto. [2]

Uchaguzi wa Raisi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 2010, wakati wa uchaguzi wa raisi nchini Guinea, alikuwa mwanamke pekee kati ya wagombea 24 waliosalia kabla ya kujiunga na Alpha Condé katika duru ya pili. [3]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. simodbt (2017-06-29). "Portrait. Hadja Saran Daraba Kaba, une dame de fer au parcours impressionnant (Par Ibrahima Diallo)". Mediaguinee.org (kwa fr-FR). Iliwekwa mnamo 2020-04-03. 
  2. Admin. "Portrait de Hadja Saran Daraba Kaba: Une dame de fer au parcours impressionnant.". Guineesignal.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-16. Iliwekwa mnamo 2020-04-03. 
  3. Admin. "Présidentielle en Guinée: la Cour suprême rend publique la liste des candidats". Iliwekwa mnamo 2020-04-03.