Héctor Rueda Hernández
Mandhari

Héctor Rueda Hernández (9 Novemba 1920 – 1 Novemba 2011) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Kolombia.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Héctor Rueda Hernández alizaliwa nchini Kolombia akapewa daraja ya upadre tarehe 15 Desemba 1946.
Aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo Kuu la Bucaramanga tarehe 5 Mei 1960 akatawazwa rasmi tarehe 19 Juni 1960. Mnamo tarehe 14 Desemba 1974, Rueda Hernández aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Bucaramanga na alihudumu hapo hadi alipoteuliwa kuwa askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Medellín tarehe 7 Novemba 1991. Alistaafu kutoka Jimbo Kuu la Medellín tarehe 13 Februari 1997.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholic-Hierarchy
- Archdiocese of Medellin (Spanish)
Alitanguliwa na Created |
Archbishop of Bucaramanga 1974–1991 |
Akafuatiwa na Darío Castrillón Hoyos |
Alitanguliwa na Alfonso López Trujillo |
Archbishop of Medellín 1991–1997 |
Akafuatiwa na Alberto Giraldo Jaramillo |