Nenda kwa yaliyomo

Gwen Mahlangu-Nkabinde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gwendoline Lindiwe “Gwen” Mahlangu-Nkabinde (alizaliwa tarehe 16 Agosti 1955) ni mwanasiasa wa Afrika Kusini aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Taifa la Afrika Kusini kuanzia mwaka 2008 hadi 2009.

Aliteuliwa kuwa Naibu Spika tarehe 23 Aprili 2004, na baadaye akachaguliwa kuwa Spika tarehe 25 Septemba 2008, akimrithi Baleka Mbete ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Raisi wa Afrika Kusini. Baadaye, nafasi yake ya Naibu Spika ilichukuliwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Nozizwe Madlala-Routledge. Kufuatia uchaguzi mkuu wa Aprili 2009, alibadilishwa kama Spika na Max Sisulu tarehe 6 Mei 2009.[1]

Mnamo tarehe 1 Novemba 2010, aliteuliwa kuwa Waziri wa Kazi za Umma, lakini aliondolewa mwaka 2011 kutokana na kuhusika kwake katika kashfa ya upangishaji wa majengo ya polisi (Police lease scandal). Kabla ya hapo, alihudumu kama Naibu Waziri wa Maendeleo ya Uchumi kuanzia tarehe 11 Mei 2009 hadi 30 Oktoba 2010.[2]

  1. ↑ "Zuma announces far-reaching cabinet reshuffle, suspends Cele". 24 Oktoba 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. ↑ "Sisulu elected National Assembly speaker". Mail & Guardian Online. 6 Mei 2009. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gwen Mahlangu-Nkabinde kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.