Nenda kwa yaliyomo

Gulf News

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gulf News
AinaGazeti la Kila Siku
MmilikiAl Nisr Publishing
MhaririAbdulhamid Ahmad
Ilianzishwa1978
Makao MakuuMakao Makuu ya Gulf News
Barabara ya Sheikh Zayed
Dubai, UAE
Uenezeshaji115,366 Kila Siku
Tovitu Rasmigulfnews.com


Gulf News ni gazeti la kila siku ya lugha ya Kiingereza inayochapishwa kutoka Dubai, katika Falme za Kiarabu lililo na wasomaji zaidi ya 115.000 kulingana na takwimu zilizokusanywa na BPA mwaka 2008. [1] Archived 4 Oktoba 2009 at the Wayback Machine. Gazeti hili lilishinda tuzo la Asia - Pacific la uzalishaji bora zaidi wa gazetti mwezi Julai 1990.

Historia ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Gulf News ilizinduliwa mara ya kwanza katika muundo wa tabloid tarehe 30 Septemba 1978 na mfanyabiashara maarufu wa UAE, Abdul Wahab Galadari; ofisi zake zilikuwa kwenye barabara ya Airport Road, Dubai. Mnamo Novemba 1984, wafanyabiashara watatu mashuhuri wa UAE, waliinunua kampuni na wakaunda kampuni ya Al Nisr Publishing. Wamiliki wapya wa jarida walikuwa Obaid Humaid Al Tayer, Abdullah Al Rostamani na Juma Al Majid. Kufuatia kifo cha Abdullah Al Rostamani mwaka 2006, nafasi yake katika bodi inashikiliwa na mchaguliwa wa familia yake wakati wakurugenzi wengine walibaki.


Chini ya umiliki mpya, Gulf News ilizinduliwa upya tarehe 10 Desemba 1985 na ilikuwa bure kwa umma. Kuanzia Februari 1986, umma ulilipishwa Dirham moja (dola senti 27) kwa paketi ya Gulf News ambayo ilikuwa na gazeti lenyewe na sehemu ndogo ya burudani iitwayo Tabloid, ambayo ilikuwa pia na matangazo.


Baada ya kuhamia makao mapya mwaka 1986, Gulf News ilianza kusambazwa katika nchi zingine za GCC: Bahrain kuanzia Septemba 1987; Oman kuanzia Aprili 1989; Saudi Arabia Machi 1989; na Qatar kuanzia Aprili 1989. Pia ikawa inapatikana nchini Pakistan kuanzia Agosti 1988. Mnamo Novemba 1995 upana wa majikaratasi ya jarida ulipunguzwa kwa sentimita nne, ili kuipa upana mpya wa kimataifa wa sentimita 38.


Al Nisr Publishing ilikuwa Kampuni yenye Madeni yenye vikwazo ikiwa na dhamani ya milioni Dh15 tarehe 26 Mei 1997.

Ofisi za Kigeni

[hariri | hariri chanzo]

Ili kutoa huduma bora kwa wasomaji wake, Gulf News ilifungua ofisi mbalimbali kote United Arab Emirates, GCC na bara-ngogo yake. Ofisi ya Abu Dhabi ilifunguliwa mwaka 1982; ofisi ya Bahrain mwezi Januari 1988; ofisi ya Oman mwaka 1989; ofisi ya Manila mwezi Agosti 1990; ofisi ya Al Ain mwaka 1994; ofisi ya Sharjah mwezi Mei 1995; na ofisi ya New Delhi mwezi Novemba 1995.


Toleo la kwanza la Gulf News kwenye tovuti lilizinduliwa tarehe 1 Septemba 1996.


Gulf News walihamia kwenye makao yao makuu ya sasa katika Barabara ya Sheikh Zayed tarehe Aprili 2000. Makao makuu ya sasa yako na vifaa vya kisasa kila mahali, pamoja na mtandao wa fiber-optic na moja ya vituo vya uchapishaji vyenye teknolojia ya hali ya juu kabisa katika Mashariki ya Kati.

Udhamini & Uendelezaji

[hariri | hariri chanzo]

Gulf News ilikuwa gazeti la kwanza katika kanda kuendeleza sanaa, utamaduni, muziki na michezo kupitia udhamini wa matukio. Mnamo Machi 1989 Gulf News ilianza Ghuba Business Awards kwa kushirikiana na DHL kwa CEO bora zaidi na mfanyibiashara. Mradi huu ulikomeshwa mwaka 1996.


Tukio maarufu la News Fun Drive ulianza Machi 1986. Tukio la Fun Drive la 26 lilifanyika mwezi Desemba 2006 na uliona magari 750 na zaidi ya washiriki 2800.


Tukio lingine kubwa ni Mashindano ya kombe la Dunia ya Farasiya dola milioni 6, ambalo hujumuisha mashindano saba bora na hujumuisha shindano la farasi wa Waarabu 'Purebred'. Gulf News linadhamini shindano la dola milioni 2 la Dubai Golden Shaheen, mbio za kikundi cha kwanza ambalo ni vutio kuu, katika mkutano. Gulf News pia hudhamini shindano nzima la jioni la farasi huko Nad Al Sheba, na kila mbio hupewa jina baada ya gazeti yao moja.


Jarida pia hudhamini idadi ya matukio ya michezo nyingine kubwa katika UAE, vilevile semina na mikutano. Maarufu kati ya haya ni Mkutano wa Mikakati ya Kiarabu, ambapo viongozi katika sekta ya siasa hukusanyika kujadili matukio yanayoathiri kanda.

Jukumu katika Kupigwa marufuku kwa Orkut

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 3 Julai 2007, Gulf News walirejerea suala la "shughuli zisizo na maadili" za jamii za Orkut, makichapisha malalamiko kutoka kwa wanachama wa jumuiya ya umma dhidi ya jamii za Orkut kama "Dubai Sex", na kuleta malalamiko rasmi kwa shirika la mtandao la Etisalat [1]. Hofu ya maadili iliyofuata ilifanya kupigwa marufuku upya ka tovuti hiyo na Etisalat tarehe 4 Julai 2007 [2]

Makanushi ya Holocaust

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 4 Januari 2009, makala iliyochapishwa na Dr Muhammad Abdullah Al Mutawa, wa sosholojia katika Chuo Kikuu cha Al Ain UAE ambayo ilisema kwamba Nazi "Holocaust ilikuwa uwongo tu uliokuwa uumebuniwa na Zionists ili kusaliti ubinadamu." Iliendelea "Ni dhahiri kwamba ilikuwa ni njama iliyopangwa na Zionists na Nazis, na watu wengi wasio na hatia walitoa maisha yao kutokana na njama hii ya unyama." Wahariri baadaye walisema ilikuwa utafsiri mbaya kutoka Kiarabu.

  1. [2] ^ Orkut.com 'yatumiwa kwa shughuli zisizo na maadili' Archived 2 Mei 2009 at the Wayback Machine. Gulf News 3 Julai 2007
  2. [3] ^ Orkut.com kupigwa marufuku katika UAE Archived 28 Februari 2009 at the Wayback Machine. Gulf News 4 Julai 2007

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]