Gregorio Pietro Agagianian
Mandhari
Gregorio Pietro XV Agagianian (15 Septemba 1895 – 16 Mei 1971) alikuwa kardinali wa Kiarmenia katika Kanisa Katoliki. Alikuwa mkuu wa Kanisa Katoliki la Armenia (kama Patriarki wa Kilikia) kuanzia mwaka 1937 hadi 1962 na alisimamia kazi za umisionari za Kanisa Katoliki lote kwa zaidi ya muongo mmoja hadi alipostaafu mwaka 1970.
Alizingatiwa kuwa miongoni mwa walioweza kuchaguliwa kuwa Papa mara mbili, mwaka 1958 na 1963.[1]
Tarehe 28 Oktoba 2022 huko Roma imeanza kesi ya kumtangaza mtakatifu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |