Grace Wahu
Mandhari
Grace Wahu Kenyatta (1897 – 4 Aprili 2007) alikuwa mke wa kwanza wa Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa Kenya. Rekodi zinaonyesha kwamba Wahu alioana na Kenyatta, wakati huo akijulikana kama Johnstone Kamau, karibu mwaka 1917 au 1919. Wawili hao walikuwa na watoto wawili: Peter Muigai Kenyatta (1922–1979) na Margaret Wambui Kenyatta (1928–2017).
Grace Wahu alifariki dunia tarehe 4 Aprili 2007 akiwa na umri wa miaka 110.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Muthoni, Kamau. "Wahu Kenyatta's land left to church, daughter". The Standard.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Grace Wahu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |