Gorreth Namugga
Gorreth Namugga ni mwanasiasa wa nchini Uganda. Mnamo 2021 alichaguliwa kama Mbunge wa kaunti ya Mawogola, wilaya ya kusini kupitia tiketi ya chama cha National Unity Platform . [1][2] Anatoka katika chama kikuu cha upinzani, National Unity Platform. Pia ndiye mwanasiasa wa kwanza wa upinzani kushinda nafasi ya Ubunge katika wilaya ya Sembabule tangu mwaka 1986.[3]
Uzoefu wa kazi
[hariri | hariri chanzo]Alifanya kazi kama Mwenyekiti wa Tume ya Huduma ya Wilaya na pia alikuwa Mmiliki wa Shule huko Sembabule.[1] Alikuwa Afisa Mkuu wa Ununuzi wa zamani wa jiji la Masaka.[1]
Majukumu ya Bunge
[hariri | hariri chanzo]Namugga kwa sasa anafanya kazi kama waziri kivuli wa Sayansi, katika Ubunifu na Teknolojia.[4] Namugga aliandaa na aliwasilisha ripoti ya wachache kuhusu bajeti ya mwaka wa 2022/2023.[5] Pia anafanya kazi kama Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Umma (PAC).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 "The women who trounced men in parliamentary races". New Vision (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-08.
- ↑ "Namugga Gorreth - 2021 General Election - Visible Polls". visiblepolls.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-10.
- ↑ "I'm focused on uprooting NRM from Sembabule - NUP MP - The Witness" (kwa American English). 2021-01-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-10-19. Iliwekwa mnamo 2022-03-08.
- ↑ Wadero, Arthur Arnold (2021-06-28). "Uganda: Nup Runs Away With Shadow Cabinet Posts". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-08.
- ↑ "Uganda: MPs approve Budget Framework Paper in readiness for FY 2022/23 Budget". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-03-08. Iliwekwa mnamo 2022-03-08.