Goretti Kyomuhendo
Goretti Kyomuhendo ni mmoja wa waandishi mashuhuri wa riwaya kutoka Uganda, na mwanzilishi na mkurugenzi wa African Writers Trust pamoja na TUBAZE African Books. Ameandika riwaya tano: The First Daughter (1996); Secrets No More (1999), iliyoshinda tuzo ya Uganda National Literary Award kama riwaya bora; Waiting (2007), iliyochapishwa na The Feminist Press huko New York na baadaye kutafsiriwa kwa Kihispania; Whispers from Vera (2023); na Promises (2025), iliyochapishwa na Catalyst Press nchini Marekani.[1]
Mwaka 2014 alichapisha kitabu The Essential Handbook for African Creative Writers. Pia ameandika vitabu kadhaa vya watoto na hadithi fupi.
Kyomuhendo ana shahada ya uzamili katika Uandishi wa Ubunifu (Creative Writing) kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, ambapo pia aliwahi kufundisha somo hilo. Alikuwa mwanamke wa kwanza kutoka Uganda kupata ushirika wa International Writing Program kutoka Chuo Kikuu cha Iowa. Kazi yake kama mwandishi na mwanaharakati wa fasihi imetambuliwa kimataifa. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa jopo la majaji wa Caine Prize na kuhudumu kama jaji wa Commonwealth Book Prize.
Mwaka 2019 alitajwa kuwa mmoja wa Waafrika 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi na jarida la New African.
Ni mmoja wa waanzilishi wa FEMRITE (Chama cha Waandishi Wanawake Uganda) na aliwahi kuwa mkurugenzi wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka kumi. Pia alikuwa Mratibu wa Programu wa kwanza wa FEMRITE kuanzia mwaka 1997 hadi 2007. Alianzisha African Writers Trust mwaka 2009 baada ya kuhamia London, Uingereza mwaka 2008.[2]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Maria Goretti Kyomuhendo alizaliwa na kukulia mjini Hoima, mji uliopo Magharibi mwa Uganda. Alipata shahada ya Bachelor of Arts (Hons) katika Masomo ya Kiingereza (2003) kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban, Afrika Kusini, na Shahada ya Uzamili ya Master of Arts katika Uandishi wa Ubunifu (Creative Writing, 2005) kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban. Mwaka 2003, Kyomuhendo alipewa Graduate Scholarship kwa ubora wa kitaaluma na Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal. Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Uganda kupewa heshima ya Honorary Fellow in Writing katika Chuo Kikuu cha Iowa mwaka 1997, baada ya kushiriki katika International Writing Program ya Iowa.[3][4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Promises by Goretti Kyomuhendo". Catalyst Press. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)[dead link] - ↑ "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Machi 2012. Iliwekwa mnamo 25 Agosti 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link) CS1 maint: bot: original URL status unknown (link) CS1 maint: date auto-translated (link), Internationales Literaturfestival Berlin. Retrieved 24 August 2011. - ↑ Lamwaka, Beatrice. "Goretti Kyomuhendo of African Writers Trust" Archived 20 Julai 2011 at the Wayback Machine, AfroLit, 22 May 2011. Retrieved 24 August 2011.
- ↑ Lamwaka, Beatrice. "Goretti Kyomuhendo" Archived 16 Agosti 2011 at the Wayback Machine, Mosaic: literary arts of the diaspora, 13 December 2008. Retrieved 24 August 2011.
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Goretti Kyomuhendo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |