Gonsalo Da Silveira
Mandhari

Gonsalo Da Silveira, S.J. (23 Februari 1526 - 1561) alikuwa padri mmisionari Mjesuiti kutoka Ureno aliyefika Msumbiji tarehe 11 Machi 1560 baada ya kuongoza miaka mitatu shirika lake huko India. Baada ya kumbatiza chifu wa Wakaranga na watu wake 450 akaendelea kuhubiri sehemu za ndani ya Afrika akafika Manica (mji mkuu wa Ufalme wa Mutapa) tarehe 26 Desemba 1560.
Baada ya kuhubiri kwa muda wa majuma matatu Mwene Mutapa (mfalme) alipokea ubatizo pamoja na wakubwa 300. Lakini washauri wake Waislamu wakamshtaki Da Silveira kuwa mpelelezi na mchawi. Hapo Mwene akageuka akamwua Da Silveira alipolala usingizi. Maiti yake ikatupwa mtoni [1].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ John Baur, 2000 Years of Christianity in Africa, toleo la pili, Nairobi 2009, kur. 79-81
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Chadwick, Life of the Ven. Goncalo Da Silveira (Roehampton, 1910);
- Theal, Records of S. E. Africa, printed for the Government of Cape Colony, VII (1901);
- Wilmot, Monomotapa T. F. Unwin (London, 1896)
- Appendix C includes a translation of Bib. Vat. Cod. Othob. Lat. 2416, F 899. (1699/1700).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |