Goliathi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Goliati)
Daudi na Goliati kadiri ya Osmar Schindler (1888 hivi).

Goliathi (kwa Kiebrania גָּלְיָת, Golyat; kwa Kiarabu جالوت , Ǧulyāt) alikuwa jitu[1] la kabila la Wafilisti ambaye habari zake zinasimuliwa na Biblia na Kurani.

Kitabu cha Kwanza cha Samueli sura ya 17 kinasema kijana Daudi alishindana naye akitumia kombeo na mawe akafaulu kumshinda na kumuua. Habari hii ya kusisimua imejulikana sana ikileta ujumbe wa kwamba wasio na uwezo wa kwao kwa nia imara na kwa msaada wa Mungu wanaweza kushinda wanaowazidi.

Hata hivyo Kitabu cha Pili cha Samueli 21:19 kinamtaja Elhanan bin Jair kama muuaji wa Goliathi[2]. Tofauti hiyo inatokana na jinsi vitabu hivyo viwili vilivyotungwa kwa kukusanya mapokeo yoyote juu ya mwanzo wa Ufalme wa Israeli bila kuyachambua[3].

Goliathi anatajwa pia katika Qur'an (2: 247–252)[4].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Hays, J. Daniel (December 2005). "Reconsidering the Height of Goliath" (Portable Document File). Journal of the Evangelical Theological Society 48 (4): 701–14. 
  2. Halpern, Baruch (2003). David's Secret Demons: Messiah, Murderer, Traitor, King (in English). Wm. B. Eerdmans Publishing. p. 7-10. ISBN 9780802827975. 
  3. The most widely accepted explanation is that the storytellers have displaced the deed from the obscure Elhanan to the more famous character, David. David's Secret Demons, Baruch Halpern, (2004), p. 8
  4. Encyclopedia of Islam, G. Vajda, Djalut

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Goliathi kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.