Glory Edim
Glory Okon Edim ni mwandishi na mjasiriamali wa Nigeria na Marekani. Anajulikana zaidi kama mwanzilishi wa mtandao wa usomaji wa vitabu unaoitwa Well-Read Black Girl. Alipokea Tuzo ya Innovator’s Award ya Los Angeles Times Book Prize mwaka wa 2017 kutokana na mchango wake katika kukuza usomaji na jamii ya wasomaji.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Edim alizaliwa na kukulia Arlington, Virginia, Marekani, akiwa mtoto wazazi wake walikuwa wahamiaji kutokanchini Nigeria waliopitia vita vya Biafra. Baba yake alirudi nchini Nigeria mapema miaka ya 1990; akiwa bado mdogo, Edim na mama yake walimfuata huko nchini Nigeria, lakini baadaye walirudi nchini Marekani kutokana na udhaifu wake aliokuwa nao. Mama yake, ambaye mwanzo alikuwa mwanahistoria, alisoma tena na kuwa muuguzi.
Alisoma katika Trinity College kwa ufadhili wa masomo kabla ya kuhamia Howard University, ambako alisomea maswala ya uandishi wa habari.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Edim alianzisha Well-Read Black Girl (WRBG) kupitia Instagram mwaka wa 2015 alipohamia jiji la New York City. Mradi huu ulianza kama ukurasa wa mitandao ya kijamii uliokuwa ukichapisha picha na nukuu za waandishi wanawake Weusi, ukiwa na lengo la kujenga jamii ya wanawake Weusi wanaopenda vitabu na majadiliano ya fasihi.
Baadaye alianzisha klabu ya vitabu Brooklyn ambapo waandishi mbalimbali walihudhuria, na hatimaye akaanzisha tamasha la fasihi la WRBG mwaka wa 2017 lililofanyika Brooklyn na kuuzwa tiketi zote.
Mnamo Mwaka 2018 alichapisha kitabu cha mkusanyiko wa maandiko kinachoitwa Well-Read Black Girl: Finding Our Stories, Discovering Ourselves. Kitabu hicho kilipokea mapokezi mazuri ya kitaaluma na kimechukuliwa kama mchango muhimu katika fasihi ya wanawake Weusi.
Vitabu
[hariri | hariri chanzo]- Well-Read Black Girl: Finding Our Stories, Discovering Ourselves (2018)
- On Girlhood: 15 Stories from the Well-Read Black Girl Library (2021)
- Gather Me: A Memoir in Praise of the Books That Saved Me (2024)
Tuzo na heshima
[hariri | hariri chanzo]- Innovator’s Award, Los Angeles Times (2017)
- Hurston/Wright Merit Award (2019)
- NAACP Image Awards – uteuzi wa kazi bora ya uandishi (2019)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Glory Edim kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |