Glaucoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Macho ya mtu mwenye glaucoma.

Glaucoma ni ugonjwa unaosababishwa na uharibifu wa jicho.

Ugonjwa huu husababishwa na shinikizo linaloongezeka katika jicho. Shinikizo hilo husababisha uharibifu wa mishipa ya optic (optic nerves) katika jicho. Hii inaweza kusababisha upofu na maumivu makali katika jicho.

Wakati mwingine ni vigumu kwa watu kugundua kuwa wana glaucoma, maono yanapotea polepole sana. Maono yakipotea kwa sababu ya glaucoma haiwezekani kurudishwa hata kwa kutumia miwani ya lenzi yoyote.

Kuna aina mbili za glaucoma, aina ambayo hutokea haraka sana, na aina ambayo hutokea polepole na kwa muda mrefu. Glaucoma ndiyo sababu ya pili ya upofu ulimwenguni. Mara nyingi glaucoma ni ugonjwa wa kurithi kutoka kwa wazazi.

Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Glaucoma kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.