Giuseppe Ceppetelli
Mandhari
Giuseppe Ceppetelli (15 Machi 1846 – 12 Machi 1917) alikuwa prelati wa Italia wa Kanisa Katoliki aliyekuwa Patriarki wa jimbojina la Konstantinopoli kutoka 1903 hadi kifo chake.
Alipadrishwa katika Jumamosi Kuu ya mwaka 1870 akapewa daraja ya uaskofu mwaka 1882 na Raffaele Monaco La Valletta, Makamu wa Jimbo la Roma. Tarehe 10 Agosti 1904, alimpa daraja ya upadri kijana mwenye umri wa miaka 22, Angelo Giuseppe Roncalli, ambaye baadaye alikuja kuwa Papa Yohane XXIII.
Alifariki siku moja kabla ya kutimiza miaka 71 mwaka 1917 na alizikwa mjini Roma.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Netton, Ian Richard (2006-12-22). Islam, Christianity and Tradition: A Comparative Exploration (kwa Kiingereza). Edinburgh University Press. uk. 118. ISBN 978-0-7486-3025-7.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |