Nenda kwa yaliyomo

Giovanni Antonio Guadagni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Giovanni Antonio Guadagni, O.C.D. (jina la kitawa: Giovanni Antonio di San Bernardo; 14 Septemba 1674 – 15 Januari 1759) alikuwa mtawa wa Wakarmeli Peku (Discalced Carmelite) na kardinali wa Kanisa Katoliki.[1]

Alipanda ngazi haraka ndani ya Kanisa baada ya mjomba wake kuwa Papa Klementi XII. Mapema aliteuliwa kuwa kardinali na alihudumu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Curia ya Roma.

Mchakato wa kumtangaza mwenye heri ulianza mara baada ya kifo chake, lakini ulisimama kwa muda mrefu hadi ulipoanza tena mwaka 1940. Hata hivyo, hadi sasa mchakato huo umesimama tena.

  1. Salvador Miranda. "The Cardinals of the Holy Roman Church - Biographical Dictionary - Consistory of September 24, 1731". www2.fiu.edu. Iliwekwa mnamo 2025-02-20.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.