Nenda kwa yaliyomo

Gianluca Zambrotta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gianluca Zambrotta

Amezaliwa 19 Februari 1977 (1977-02-19) (umri 49)
Como, Italia
Nchi Italia
Urefu 1.81 m

Gianluca Zambrotta (alizaliwa 19 Februari 1977) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Italia aliyecheza nafasi ya beki wa pembeni au kiungo wa pembeni pande zote mbili, kushoto na kulia.[1]

Kazi ya Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Zambrotta alianza kazi yake ya soka katika klabu ya Como mwaka 1994, kabla ya kuhamia Bari ambapo alionyesha kiwango cha juu kilichomfanya asajiliwe na Juventus mwaka 1999. Katika kipindi chake cha miaka saba na Juventus, alishinda mataji mawili mtawalia ya Serie A na Supercoppa Italiana mwaka 2002 na 2003, pamoja na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA mwaka 2003.

Baadaye alicheza katika klabu ya FC Barcelona kati ya mwaka 2006 na 2008 , kabla ya kurejea Italia kujiunga na AC Milan, ambapo alishinda taji lake la tatu la Serie A na Supercoppa Italiana mwaka 2011. Alimaliza kazi yake ya soka katika klabu ya FC Chiasso ya Uswisi mwaka 2014, timu ambayo pia alikuja kuifundisha kama kocha.

Kazi ya Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Katika ngazi ya kimataifa, Zambrotta alicheza mechi 100 katika timu ya taifa ya Italia. Alishiriki katika mashindano matatu ya Kombe la Dunia la FIFA, mashindano matatu ya kombe la ulaya, na Michezo ya Olimpiki ya Mwaka 2000. Alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2006, na alichaguliwa kwenye kikosi cha wachezaji bora wa mashindano hayo.

  1. ↑ "Gianluca Zambrotta". AC Milan. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Juni 2012. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gianluca Zambrotta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.