Giacomo Tedesco
Makala hii inahitaji vyanzo zaidi ili kuwezesha kuonyesha uthibitisho. |
| Giacomo Tedesco | ||
| Maelezo binafsi | ||
|---|---|---|
| Jina kamili | Giacomo Tedesco | |
| Tarehe ya kuzaliwa | 1 Februari 1976 | |
| Mahala pa kuzaliwa | Palermo, Italia | |
| Urefu | 1.75m | |
| Nafasi anayochezea | Mchezaji wa kati | |
| Maelezo ya klabu | ||
| Klabu ya sasa | Reggina | |
| Namba | 19 | |
| Klabu za ukubwani | ||
| Miaka | Klabu | |
| 1994-1997 1997-2002 2000-2001 2003 2003-2007 2007-2009 2009 2010-2013 |
Palermo FC Salernitana → Napoli (mpango wa mkopo) Cosenza Reggina Catania Bologna FC [Reggina | |
|
* Magoli alioshinda | ||
Giacomo Tedesco (amezaliwa Palermo, 1 Februari 1976) alikuwa mchezaji wa kandanda wa Italia ambaye alicheza kama kiungo katika ligi za Italia. Kwa sasa ni kocha.
Wasifu wa klabu
[hariri | hariri chanzo]Giacomo Tedesco alianza kucheza katika klabu yake ya nyumbani ya Palermo FC mwaka wa 1994. Alicheza katika mji wa Palermo kwa misimu mitatu akicheza katika mechi takriban 70 na kufunga mabao matatu. Katika mwaka wa 1997, alihamia klabu ya Salernitana, alipokwenda na kucheza katika mechi 133 na kufunga mabao 13 kati ya miaka ya 1997 na 2007. Alihamia klabu ya Napoli katika msimu wa 200-2001. Katika miezi sita na klabu hiyo ya kusini mwa Italia, alicheza katika mechi 14. Katika mwaka wa 2003, alihamia kwa muda mfupi klabu ya Cosenza ambapo alifunga bao moja katika mechi 14. Baadaye mwaka wa 2003, alitia saini mkataba na klabu ya Reggina Calcio, alikocheza kwa miaka minne katika Ligi Kuu ya Italia. Alicheza zaidi ya mechi 120 katika klabu ya Reggina huku akifunga mabao 5. Katika mwaka wa 2007, licha ya kuwa na mafanikio katika mji huo wa Calabria, Tedesco alihamia klabu ya Sisilia ya Calcio Catania. Tangu kujiunga na Catania, alicheza katika mechi 50 na kufunga mabao manne katika misimu miwili. Alipokuwa na makocha, Walter Zenga na Silvio Baldini Tedesco, alikuwa akicheza mara kwa mara na alikuwa mchezaji wa bidii sana upande wa kushoto wa uwanja. Tarehe 9 Julai 2009, huduma za Tedesco ziliuziwa klabu ya Bologna FC iliyokuwa na mkataba na Tedesco wa urefu wa miaka miwili. Mnamo tarehe 14 Januari 2010, Tedesco alirudi Reggina kwa mpango uliopea Bologna Antonio Busce.
Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Kaka yake, Giovanni Tedesco alicheza naye katika timu moja katika msimu wa 1997-98 katika klabu ya Salernitana.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- archiviostorico.gazzetta.it (Kiitalia)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Giacomo Tedesco kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |